Mchungaji Florian katunzi akiwa na kijana aliyekuwa mwizi na kunusurika kuuwawa zaidi ya mara tatu na mtoto Husna ambaye alikuwa akianguka kila akienda shuleni na sasa amefunguliwa yupo huru.
mchungaji Katunzi akiwa na kijana Idrisa ambaye alikuwa mwizi na kufika kanisani alifunguliwa na kuwekwa huru na sasa ni mzima anendelea vizuri.
Ni nyama ambaye ametapika mmoja wa watui walofika kanisani hapo kutafuta msaada baada ya kuteseka kwa muda mrefu bila mafanikio na sasa amefunguliwa yupo huru
Umati wa waumini waliohudhuria ibada ya maombi na maombezi kipengele cha uweza na nguvu.
waumini wakifurahia neno la Mungu kanisani EAGT City Center wakati mchungaji Katunzi hayupo pichani akifundisha somo la maombi na maombezi kipengele cha uweza na nguvu.Waumini wakishangilia kwenye ibada ya neno la Mungu ndani ya kanisa la EAGT City Center,
Hali imeelezwa kuwa ya tofauti sana pale watu
mbalimbali wa dini na madhehebu mbalimbali kufika katika kanisa la EAGT City
Center na kufunguliwa na kuwekwa HURU mbali na magonjwa .
Hayo yamesemwa na mchungaji kiongozi wa kanisa
hilo mchungaji Florian Katunzi wakati akifundisha somo la Maombi ndani mwa
maombi kipengele cha Uweza na nguvu ambapo alinukuu kitabu cha Isaya 40:27-31 ambayo
inasema Mbona
unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana
asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua?
Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala
hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa
nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na
kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana
watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala
hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Aidha amesema kuwa lengo la siku hizi 90 ni
kuwafikia watu wengi wa dini mbalimbali na madhehebu mbalimbali ili waweze
kufunguliwa.
"Ila upinzani unainuka kwa njia nyingi ili
usihudhurie ibada ya siku 90 ila unawezuiliwa na dini sasa imefika wakati wa
kuvuka mipaka ya dini dhehebu ili uwekwe huru'alisema mchungaji Katunzi.
Aliongeza kuwa
akili za Mungu hazichunguziki maana anampa nguvu na uwezo wewe usiye na
nguvu wala uwezo maana Mungu ni mwenye uwezo na anaweza kuzipindua nguvu za
giza , wachawi na waganga ili watu wa Mungu wainuliwe na uzao wa mwanamke
usiendelee kuteseka na kutaabika.
Alinukuu
kitabu cha Yoshua 6:1 na kusema kuwa Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa
Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia.
"Uzao wako unaweza kufungwa ili kisiwepo
kinachoingia wala kutoka maana kila kizuizi kilichowekwa kinaondoshwa kwa jina
la Yesu",aliongeza mchungaji katunzi.
Alisema kuwa kitabu cha Yoshua 5:13-14
kinasema, Lazima ufahamu kuwa kuna adui wanaokuzunguka na wanatafuta njia ya
kukuangamiza wa kusimama mbele zako maana Mungu wako yupo ambaye anaenda kukuokoa
na kukuweka huru.
Uwezo
wa kumiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho na mwili uko ndani yetu maana Uwezo
huu u juu ya ufalme wote na mamlaka,tangu mwanzo wa mwanadamu Mungu alimpa
uwezo na nguvu za kiutawala ambapo maandiko yanasema; katika Mwanzo 1:21-28“Mungu
akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa
baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba,
Hata
hivyo Mungu aliweka nguvu ya kutawala ndani ya mwanaume na mwanamke ambapo kuna
funguo kumi na saba za kufungua njia hivyo njia iliyofungwa lazima ifunguliwe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni