Wapambe wa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa
wamefanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM, makao makuu ya CCM wakipinga
Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora.
Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alithibitisha Dk
Asha Rose Migoro, Dk Pombe John Magufuli, Benard Membe, Januari Makamba na
Balozi Amina Salum Alli kupenya katika tano bora kati ya wagombea 38
waliojitokeza kuwania nafasi ya kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.
Wapambe hao walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama
cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho sio cha kindugu na pia sio cha
kifalme.
Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema hali si shwari mkoani
Dodoma ambapo sintofahamu imetawala kuhusiana na Edward Lowassa kukatwa.
Bado haijulikana nini hatma ya kikao cha Halmashauri Kuu
kinachoendelea kwa kuwa wajumbe wengi wanapinga Lowassa kuchujwa.
Wajumbe hao waliimba nyimbo ya kuonesha kuwa na imani na
Lowassa, wakati Rais Jakaya Kikwete na marais wastaafu wakiingia ukumbini.
“Tuna imani na Lowassa, oyaa, oyaa, oyaa, Lowassa oyee,
oyee…oyee…oyee…oyee oyee Lowassa, Lowassa safi, safi……”
Rais Kikwete na viongozi wengine walijikuta katika mazingira
yaliyowalazimisha kuimba wimbo huo, tofauti na matarajio yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni