YESU NI JIBU

Jumapili, 5 Julai 2015

ASKOFU MKUU NA MWANZILISHI WA KANISA LA CATHEDRAL OF JOY (COJ), APOSTLE JOHN KOMANYA, AMEFARIKI DUNIA KWENYE HOSPITALI YA HINDU MANDAL, JIJINI DAR ES SALAAM.

Taarifa ambazo zimetufikia alfajiri ya leo na kisha kuthibitishwa punde, zinaeleza kwamba Askofu Mkuu na mwanzilishi wa kanisa la Cathedral of Joy (CoJ), Apostle John Komanya, amefariki dunia alfajiri ya saa kumi kwenye hospitali ya HIndu Mandal, jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli, ameieleza GK kwamba Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa Hospitali ya Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata ahueni. 


Siku mbili nyuma ndipo alipozidiwa tena na hivyo kupelekwa Hospitali ya Hindu Mandal, ambapo mauti yalimkuta hapo. Marehemu ameacha mke na watoto 3 ambao wako nchini Marekani, sehemu ambayo pia alikuwa akihudumu. 

Kwa sasa ratiba za ibada ya kanisa la CoJ ambalo lipo Gogoni Kiluvya, zimehamishiwa kwa dada wa marehemu, Makoka, ambapo ibada huanza saa nne asubuhi. 

Picha mbalimbali za Apostle John Komanya enzi za uhai wake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni