YESU NI JIBU

Alhamisi, 23 Julai 2015

ANANIA MWASOMOLA AWATOLEA UVIVU WAPENDWA WANAOHUKUMU WAIMBAJI WANAOTUMIKA KATIKA KAMPENI ZA KISIASA.

Biblia katika kitabu cha Wagalatia 3:1-14 inaelezea vyema,ndugu msomaji unaweza ukasoma na kupata ufahamu juu ya imani ya kumtegemea Mungu(Roho Mtkatifu) katika maisha yako ya kila siku bila kuyumbishwa na kitu chochote maana Roho Mtakatifu atakuongoza nini cha kufanya na kutofanya.
Hali imekuwa ya tofauti katika ulimwemungu wa sasa na nini hasa sababu ya hali hii ni waumini kutofahamu ama kutokuwa na uongozi wa Roho Mtakatifu wameweka mahitaji mbele kuliko kuliko MUNGU.
Sasa msomaji wangu hapa tuungani na ndugu ANANIA MWASOMOLA
 anavyozungumza juu ya wapendwa wanohukumu waimbaji wa njyimbo za injili ambao walitumika katika kampeni za siasa.
Nimesoma miaka mitatu mliman nikisomea political science leo hii unategemea ntafanya Kazi gani? .
Uimbaiji nikazi kama walivyo wachungaji na wengine watumishi wa Mungu
Matusi yenu siyaogopi wala waimbaji wenzangu hawababaishwi kwa hilo ila hivi mnajua kuwa mnahukumu akati ninyi sio watoa hukumu? Na nani mtakatifu kati yenu amini nawaambieni uimbaji unanguvu kuliko chochote hapa Duniani nandiyo mana Mungu anapenda sifa kuliko jambo lolote.
Ushauri wangu ukiona waimbaji wanakukwaza acha kuwaskkiliza kwani umelazimishwa kuwasikiliza alafu nyie walokole ndiyo mnaongoza kwakubani CD zawaimbaji na kuweka kwenye cm zenu nyimbo tena huwa hamnunui CD original mnanunua feki.
Acheni matusi nyie kama mnajiona mnajua kuimba tungeni nyimbo tuwasikie mana nyie ndiyo watakatifu wengine wadhambi yaani mmejaa unafki tu mnahukumu nyie Mungu?
Anataka waimbaji waje kula kwenu hivi hamuwazi kuwa waimbaji nibinadamu na wanamahitaji kama wengine kanisani wakiomba hela mnasema wanapenda hela sasa wako kutafuta bado matusi acheni unafki wenu naongea kwani mnakera na maneno yenu hayatunyimi usingizi.
Usipowapenda waimbaji wewe jua niwewe wapo wanaojua umuhimu wawaimbaji hawa.
Hapo ulipo unanyimbo za waimbaji hawa alafu unaleta unafki kusema hawajaokoka kwani wewe nani uhukumu?
Mbona wachungaji wamegawanyika kwenye siasa kila mtu anamsifia mwanasiasa wake hamjawaona ila waimbaji ndiyo mume waona? Nendeni zenu na msipo tupenda ninyi wapo wanao heshimu hii huduma.
Uimbaji ni huduma tena ni kipaji kama hamuamini anza kuimba leo maana huwa mnadhani kuimba nikulima shamba ingieni muone.
Wewe unayesema waimbaji wa Marekani hawawasifii wanasiasa hivi wewe mzima? Mbona mnafki tena muongo uchaguzi wa Obama wewe uliona kampeni zake nani aliimba wimbo wa America we trust you Barack? Au mnadhani hatufatilii wenzetu au unadhani wote tuna elimu kama zako
Semeni mpaka mchoke ila uimbaji ni kipaji Mungu anagawa kwa wenye uwezo ukiona upo upo ujue Mungu hajakujalia baki na unafki wako
Walokole hamtaingia mbinguni kwa dhambi ya unafki maneno maneno umbea umewajaa.
Kwaniaba ya waimbaji wote nasema semeni muwezavyo ila bila waimbaji hakuna injiri Duniani kote Mungu anaakiri kuliko wewe ndiyo maana anaweka uimbaji sasa wewe hujui lolote eti waimbaji wanapenda pesa umbea tu nani hapendi pesa dunia hii.
Wanafiki wote mbingu haiwahusu kaeni na lawama zenu nawatia moyo ndugu zangu waimbaji fanyeni Kazi ya Mungu vema na mkumbuke watoto waende shule Mc Joshua Makondeko Chris Mwahangila Emanuel Mabisa Bahati Bukuku na wengine wengi Leah Mwankundile Ammy Mwakitalu Mtume Kijana Bashando Gazuko Junior.
maneno hayo nimechukua kwenye facebook,Je wewe ndugu msomaji mpendwa wa blog hii unaonaje ni sahihi kumwimbia mtu hata kama ni siasa ama.
wasiliana nasi kwa whatsapp 0752834514 au piga 0779632616 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni