·
Kanuni ya Mungu ni kupanda na kuvuna
(Isaya 6:8)
Katika mfululizo wa makala haya,
tumekuwa tukijifunza umuhimu wa kujitolea muda wetu, mali zetu na akili zetu
kumtumikia Mungu kama alivyotuagiza katika Neno lake. Leo Mtumishi wa Mungu,
Mchungaji Florian Josephat Katunzi, anaeleza
kwa kina umuhimu wa kila aliyeokolewa kuamka na kwenda kumuokoa mwingine
anayeangamia dhambini, kuzimu ikipanua mdomo kumdaka. Tafadhali ungana na
Yonathan Landa katika makala haya...
Jukwaa ambalo mtumishi wa Mungu mch.Florian Josephat Katunzi analihitaji kwa ajili ya kazi ya MUNGU ya kueneza injili kwa watu wote.
Yapo maswali makuu anayouliza Bwana kwetu sisi tunaolicha
jina lake. Maswali yenyewe ni haya; 1. Nimtume nani? Hapa Muumba wetu, akiisha
kutuokoa kwa damu yake ya thamani atutaka tusikae chini na kufikiri tumefika.
Laa anataka mtu wa kumtuma kuwaendea wale wengine ambvao bado wanamtumikia
shetani.
Ni hapa swali libngine linapokuja kwetu, Je ni nani
atakayekwenda kwa ajili yetu. Bwana anamtafuata mtu atakayemtuma kumletea
wanakondoo wengine waliopotea. Anawahitaji zizini mwake.
Inatupasa hapa kukumbuka kuwa mtu huyu hatakwenda kwa
niaba yuetu tu, bali atakwenda kwa ajili yetu. Mpango wa injili wa miaka 20 unahitaji Mtu
atakayekwenda kuhubiri habari njema za
ufalme wa Mungu, mtu huyu lazima aenda kwa niaba yetu. Hivyo basi, unaposhiriki
kwa sadaka yako maana yake ni kuwa umemtuma mhubiri aende shambani mwa bwana
kwa niaba yako na watoto wako.
Mimi nilipoupokea mpango huu nilikubalia kwenda kwa ajili
yanu kuhubiri pamoja nanyi katika mpango
huu wa miaka 20 ya safari ndefu za
kuwakoa wale ambao bado hawajaokolewa ndabni na nje ya nchi yetu.
Mtumishi wa Mungu , Musaa alipokuwa kwenye misheni ya
kuiokoa wana wa Israeli kutoka utumwani Misiri aliulizwa na Farao (mtawala wa
Misri) “Utaenda na akina nani huko Jangwani kumtumikia huyo Mungu wako?”
Majibu ya maswali haya yanapatikana katika Biblia kitabu
cha Kutoka 10:9, jibu lenyewe ni hili:
“Musa akamjibu; tutakwenda na
vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda nma kondoo
zetu na ng’ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana siku kuu.”
Katika mpango huu wa wokovu inatupasa kumtumikia Mungu
sisi na watoto wetu, tutakwenda na mali zetu (sadaka zetu). Malizetu lazima
zitumike katika kazi ya Injili, tupate vyombo, gari na Jenereta.
Ni muhimu sana watoto wetu wawe sehemu ya huduma, vijana
wako wawe sehemu ya huduma ili kwa sadaka zako tuwe alama ya ukumbusho katika
Ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Leteni sadaka hizi, imje mbele zake katika utukufu ili sifa zimuendee yeye, kama maandiko
matakatifu katika zaburi yasemavyo: “Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, leteni
sadaka mkazingie nyua zake.”
(Zaburi 96:8)
Sdaka yako ni kiunganishi na Mungu aliye hai kwa kuwa
kupitia utoaji Yeye huuona unyofu wako kwake. Neno la Mungu linasema: “Ndipo
ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.”
(Mithali 3:10). Sadaka yako ya Injili itakuondolea msiba usiwe katika nyumba yako na raha siku ya
mapito yako uwe na kitu cha kumkumbusha Mungu aliye hai jkama alivyofanya Ezekia.
“Siku hizo Ezekia aliugua, akawa
katika hatari ya kufa, na Isaya mwana wa aAmuzi, akaenda kwa Mfalme,
akamwambia, Bwana asema hivi, tengeneza mambo ya nymba yako; maana utakufa,
wala hutapona . basi Ezekia akajigeuiza akaelekeza uso wake ukutani akaomba
Bwana, akasema, eeBwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako
katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyomema machiini kwako.
Ezekia akalia san asana. Ikawa neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, enenda
ukamwambie Ezekia, Bwana , Myungu wa daudi, baba yako, asema hivi, mimi
nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama nitaziongeza siku zako,
kiasi cha miaka 15.” (Isaya 38:16).
Nakaribisha
marafiki wa Injili tushirikiane ili kutimiza mpango huu ambao si wa kidhehebu
wala haufungwi na kundi lolote; tunaalika watu 200 watakaojitoa kwa sadaka ya
shilingi 1,000,000, kwa ajili ya maandalizi haya ya ununuzi wa vifaa vya
Injili, watu 200 watakaojidhabihu kwa sadaka ya shilingi 500,000. Lakini pia
tunawaalika wengine kuungana nasi kwa njia ya utoaji wa sadaka zao ili
kukamilisha mpango huu mkubwa unaolenga kufika kila kijiji cha Tanzania
kukabiliana na giza hili la kiroho.
Aina ya magari ambayo ndiyo yanahitajikwa kwa ajili ya kueneza injili kwa kusafirishia vyombo na jukwaa.
Mimi
pamoja na wewe uliyepokea neema hii ya Injili hatuwezi kutulia wakati shetani
akihubiri hadharani na kuchukua watoto wetu kila dakika wakijiunga na ibada za
kishetani kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka haraka.
Nawaomba
wana-injili watuunge mkono katika mpango huu mkubwa na maono haya, yenye lengo
la kuwafikia wenzetu kokote waliko, ili tuweze kununua vyombo hivyo, jukwaa na
gari kwa ajili ya safari za injili nchi nzima.
Unaweza
kushirikiana nasi katika mpango huu wa ki-Mungu kwa kuchangia kupitia akaunti
zetu zifuatazo:
Jina la Akaunti: Florian Josephat Katunzi
Benki: CRDB no. 01j1028426200
M-Pesa - 0754367826
Tigo Pesa: 0718-267171
Airtel money: 0784-367826
UKITAKA KUWASILIANA NASI WANABLOG HII WHATSAPP NI 0752834514.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni