YESU NI JIBU

Jumanne, 14 Julai 2015

HAYA NDIYO ANENAYO MTUMISHI PETER LUKUTA KUHUSU KINACHOENDELEA TANZANIA.

Nalishangazwa sana na baadhi ya wahubiri wa Tanzania kuacha kazi waliyoitiwa na Mungu na Kuingilia mambo yasiyowahusu kitendo cha kuacha kumhubiri Kristo na kuanza kumhubiri Mwana siasa kwa njia mbali mbali madhabahuni au kwenye Vyombo vya habari ni udhihirisho tosha kwamba Wahubiri wengi pamoja na umaarufu wao lakini bado kabisa ni wachanga sana kiroho bado wanahitaji kufundishwa miiko ya utumishi. Bado hawajui kuwa utumishi ni madhabahu na madhanahu inavyombo vilivyowekwa wakfu kwaajili ya Bwana pekee lakini wao wamevitwa vyombo hivyo ambavyo ni mikono yao na midomo yao wakaenda kuvitumia kwenye Matumizi isiyopaswa kitendo cha Mtumishi kuibuka na Kuonyesha wazi kumpigia debe Mwana siasa na kuacha kumpigia debe Yesu huko ni kukosa hekima ni sawa na Beltshaza alipovitwaa Vyombo vya hekalu la Mungu na kuvinywea pombe kitendo ambacho kilimchukiza sana Mungu kiasi cha kumwambia Ufalme wako Umepimwa na kuonekana umepungua na mwishowe Beltshaza akafa = DANIELI 5:25-30. Na leo Watumishi wengi utumishi wao Umepimwa na kuonekana kuwa umepungua wanahitaji toba maana wameanguka na huwezi kusimama mbele za adui yako ukiwa umeanguka na kutoka mikononi mwa Mungu =YOSHUA 7:11-12.
Ni mihimu sana kufahamu kwamba Mungu hamtetei mtu kwenye vita ambayo sio yeye aliyemtuma Mungu hakutetei pale ambapo sio yeye aliyekutuma kwenda kupambana Daudi shujaa wa vita kupita wote kwenye Biblia hakuwahi kwenda kupigana vita ambayo Mungu hakumtuma kwenda huko maana angethubutu kufanya hivyo basi ni wazi kwamba angeangamia na ndivyo ilivyo saisa imeua huduma za Watumishi kiroho ijapokuwa wanaonekana lakini ni sawa tu na tawi lililokatwa kwenye mti huwa halinyauki mapema lakini ndani yake halina uhai.
WAIMBAJI VIPOFU WA INJILI
Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kutunga nyimbo za kuwasifu na kuwatukuza pamoja na kuwaabudu wanasiasa mimi sijashngaaa hata kidogo sababu najua waimbaji wengi HAWAJAOKOKA HATA KIDOGO kwasababu hata wakialikwa kwenye huduma wanatanguliza kwanza pesa mbele hii inaonyesha kabisa mtu huyu hajaokoka kabisa na hana hata chembe ya hofu ya Mungu na ni mzinzi wa kawaida tu kwasabu Kama mtu haoni hofu kuuza huduma ya Mungu basi usitegemee kwamba atakuwa na hofu ya kuuza mwili wake Kama mtu haoni aibu kuomba pesa ndipo atoe huduma basi hawezi kuona aibu kutoa mwili wake kwaajili ya hizo hizo pesa na ndiyo maana waimbaji wengine wamepata umaarufu kwa njia za aibu kutokana na tamaa ya pesa sasa watu wa jinsi hiyo mimi siwezi kushangaa kuwaona wanamwimbia mwanasiasa badala ya Yesu hiyo siyoajabu kabisa na mimi sikushangazwa na hilo maandiko yanasema kila mbegu huzaa kwa jinsi yake na mfano wake sasa kama wamewaona Maaskofu wao wakiwashabikia wanasiasa madhabahuni Je na wao wafanyenini zaidi ya kufwata njia hiyo kwasabu nao ni wa mbegu hizohizo =MWANZO 1:12. Ni aibu kubwa mmeshindwa hata na waislamu hakuna kitu kibaya Kama kuzidiwa msimamo na farisayo sijawahi kuona Qaswida za waislamu zikitukuza wanasiasa lakini hawa wasanii wamezidiwa hekima hata na watu wa mataifa ama kweli Kipofu akimwongoza Kipofu wote hutumbukia shimoni. =MATHAYO 15:14.

UNABII WA UONGO ULIYOTOLEWA
Baadhi ya Watumishi walitoa unabii kuhusu Raisi ajaye Tanzania mimi siwahukumu kwa hilo kwasababu bado hatujapata Raisi na hatujui nini kitatokea kesho kwasababu bado hatujapata Raisi tutamjua baada ya uchaguzi mkuu hivyo siwezi kukata rufaa kabla ya hukumu.

Ninachozungumza ni hiki watoa unabii hawa wakiwemo Maaskofu na Manabii kila mtu amemtabiri mtu wake kuna wengine wametabiri Mwiguru. Wengine Lowasa. Wengine Membe sasa swali ni hili kuna Mungu wangapi? Maana Kila mtu anatabiri mtu wake ikionyesha ya kwamba kila mmoja wao ana Mungu wake sasa Je katika hao miungu yao ni yupi Wa kweli? Istoshe Nabii zote zilizotolewa zote zimeangalia wingu kwanza na hakuna nabii anayesubiri kuona wingu ndipo atabiri kuwa mvua itanyesha no Nabii wa kweli hasubiri kuona wingu bali kunako jua kali na ukame yeye anasema naiona mvua kubwa kesho huyo ndiyo Nabii lakini hawa wajanja wajanja waliyojivika kofia za vyeo wasivyojua maana yake wakidhania kuwa nisifa na kumbe ni kujidhalilisha tu siku zote Mwisho wao hua aibu =KUMBUKUMBU LA TORATI 13:2-5.
Watu wa jinsi hii kuna dalili kubwa kuwa wamehongwa pesa kama vile Yuda na Siku zote pesa ya aibu hupofua macho ya moyo mnyoofu wanasiasa sasa wanalidharau kanisa kwasababu pesa zao Tangia ile kashfa ya Dec iloyotukanisha kanisa hadi sasa watu bado hawajajifunza tu hivi unapotabiri kitu alafu kisitokee huwa utapata wapi ujasiri wa kusimama mbele za waumini wako? Pia hivi unapotabiri kitu alafu kisitimie je bado hukubali kuwa ulitabiri kwa akili zako? Na Kama ulitabiri kwa akili zako huku ukimsingizia Roho Je ni mambo mangapi hapo kanisani kwako uliyafanya kwa akili zako huku unamsingizia Mungu je hao waumini unawapeleka mbingu ya nani?MWENYE SIKIO ASIKIE
MAAMUZI MAGUNU
Ccm imefanya maamuzi magumu kumteua mtu ambaye hakutarajiwa Nimeipenda Staily hiyo kwasabu ndiyo njia ya Mungu Siku zote Mungu huchagua kitu kinachoonekana kimedharauliwa kimeonekana kama dhaifu naipenda sana hii njia ambayo hata Yesu aliitumia kunichagua mimi niliyeonekana kuwa dhaifu sistahili kuheshimika lakini Yesu akanichagua akanipa huduma akanipa mke mwema akaniheshimisha kwa kunitoa kwenye ulevi uasherati uvutaji wa bangi Yesu aliifanya maamuzi magumu na mimi nikakubali kufanya maamuzi magumu ya kuiacha dini yangu ya zamani ya UISLAMU na kukubali kuingia kwenye Ukristo. Isingewezekana endapo nisingefanya maamuzi magumu kuacha jina la Shabani Hamza Lukuta pamoja na kuacha ukoo wa Babu siyo jambo rahisi inahitaji maamuzi magumu na wewe Mwana wa Mungu fanya maamuzi magumu ili uone ushindi

MAGAIDI WALIFANYA MAAMUZI MAGUMU
Majuzi hapa magaidi walifanya maamuzi magumu kwa kuvamia kituo nambari moja kwa ulinzi na kinachoogopeka na majambazi kupita Vituo vyote Tanzania magaidi walifanya maamuzi magumu wakafanikiwa kuvamia na kuiba silaha za kutosha na kuua askari wote pia walipoona mwenzao pikipiki imegoma kuwaka wakafanya tena maamuzi magumu wakamwua yule mwenzao Kupoteza ushahidi

Sikiliza mwana wa Mungu Wewe usipofanya maamuzi magumu basi uwe na uhakika kuwa adui yako ndiye atafanya maamuzi magumu Askari wetu hawakufanya maamuzi magumu ya kukesha na silaha mkononi kujiandaa wakati wowote matokeo yake adui akafanya maamuzi magumu akwaua wote
WITO WANGU KWA JESHI LA POLICE
Wasiishietu kufanya maamuzi magumu kwenye kuthibiti maandamano na migomo ya vyama vya siasa na Wanafunzi wa vyuo vikuu maana kwa hapo hawajambo kurusha mabomu ya machozi na maji ya kuwasha aaaah mnaweza sasa msiishie tu kufanya hivyo kwa raia wasiyo na silaha zozote no ila pambaneni na hawa magaidi ambao nao wanaisilaha fanyeni maamuzi magumu kupambana nao maana msipofanya maamuzi magumu muwe na uhakika kuwa wao wataendelea kufanya maamuzi magumu

Mwana wa Mungu usipofanya maamuzi magumu ya kuomba kwa masafa marefu kukesha angalau mara mbili kwa wiki kufunga angalau masaa 48 kwa wiki kutoa Fungu la Kumi kwa uaminifu kutoa sadaka kubwa kubwa za kujikana nafsi Kama Ibrahimu usipofanya hivyo subiri Shetani kuna maamuzi magumu atafanya kuna matukio shetani ameyafanya kwa watu ambao hakutarajiwa na watu waliposikia walivunjika moyo sana hii yote imetokana na sisi wenyewe Watumishi kutofanya maamuzi magumu kwasababu Watumishi wengi wanajihurumia wanaipenda miili inawatawala ndiyo maana hawafanyi maamuzi magumu angalau kujifungia siku tatu tu kukaa na Mungu pekee bila kuonana na Mtu huku wakiomba kwa masafa marefu Matokeo yake shetani ndiye hufanya maamuzi na kusababisha Mungu aonekane hana nguvu. Nakushauri Mwana wa Mungu hebu Fanya maamuzi magumu usiogope kusemwa fanya jikane nafsi nampenda dada mmoja alifanya maamuzi magumu kwa kumpa gari Mchungaji mmoja na alikuwa na gari hilo hilo moja Matokeo yake akaepushwa na kifo ambacho kilipangwa na adui zake wakajitokeza na kutoa siri zote aliponishirikisha nikakwambia awasemehe kwa sababu wamebuni,

Namalizia kwa kusema usipofanya maamuzi magumu uwe na uhakika Shetani yeye atafanya kwa mawasiliano Tuma Masage Kwenye Whtsapp 0767 503054

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni