YESU NI JIBU

Alhamisi, 16 Julai 2015

UKARIMU WA MSHAURI! COUNSELING TRAINING BCIC MBEZI BEACH! NA MCHUNGAJI PETER MITIMINGI.

1. Unapaswa kuwa mkarimu na rafiki kwa mshauriwa wako. 

2. Onyesha mazingira ya makaribisho ya urafiki na upendo.

 
3. Ukarimu ni njia ya kawaida ya kuelezea uelewa na kujali


kwako kwa mshauriwa. 

4. Ukarimu huwa huonyeshwa kwa vitendo kama vile:


• Ishara zako unavyo zionyesha kwa mshauriwa.


• Mwonekano wa mwili wako ulivyo.


• Kiimbo cha sauti (tone of voice) Ikiwa ya chini sana


mshauriwa anaweza kudhani hujafurahia ujio wake. Pia ikiwa
 ya juu sana mshauriwa anaweza kukuogopa akadhani wewe ni mkali sana.

• Mguso wa mwili (unagusa wapi na unagusaje gusaje, kuna


 wengine wakisalimia nikama wanakupangusa tu kiganja

 hawakushiki vizuri ni kama wanakuona una kinyaa. Wengine 

wanakandamiza mikono ni kama mkono umekanyangwa na
 tairi ya trekta).

• Mapigo ya moyo yanakwendaje.

• Mwonekano wa uso ukoje. N.k

AFYA YA MSHAURI COUNSELING TRAINING! 

1. Kuna uhusiano mkubwa kati ya ushauri na kuwa na afya njema kimwili kama mshauri.
2. Afya ya mshauri ni ya muhimu sana katika mwonekano wa mshauri hasa kwa mara ya kwanza anapokutana na mshauriwa.
3. Kama afya yako sio nzuri ni vema ukaahirisha ushauri ili ushughulikie matengenezo ya afya yako. 
Mfano:
• Kushauri huku unakikoozi kikali inaweza kuwa kizuizi katrika kazi ya ushauri
• Kushauri huku unamafua makali inaweza kuwa kizuizi katrika kazi ya ushauri.
• Kushauri huku una tatizo la kuwashwa sehemu mbalimbali na hususani sehemu za siri na kwingineko inaweza kuwa kizuizi katrika kazi ya ushauri.
• Kushauri huku una homa au mareria kali unatetemeka.
• Kufanya huduam ya ushauri huku unajisikia mdhaifu na usiye na nguvu.
4. Kama mshauri jijengee mazoea ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
5. Ni hatari kufanya ushauri ukiwa na msongo wa mawazo (stress).
6. Ni hatari kufanya ushauri huku umetoka kuumizwa na mtu umejeruhiwa moyo.
7. Uimara wa afya ya kimwili ya mshauri inaweza kuchangia namna atakavyoongea na mshauriwa wake na namna ambavyo mshauriwa atakavyo muona mshauri.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni