YESU NI JIBU

Jumanne, 14 Julai 2015

MAGUFULI AJITAMBULISHA RASMI KWA WANANCHI WA JIJI LA DAR KATIKA VIWANJA VYA ZAKHEM.

 Ama kweli hapa sasa tunaona mtu ambaye hapo awali hakuwa anatangazwa sana wakati wa kutafuta wadhamini sasa kila kona anasikika mpaka na hata wale ambao hapo awali hawakuwa na haja naye kwa sasa kila mmoja anamwita na kutamani kusalimiana naye na pia kama inawezekana apate hata dakika kadhaa za kuzungumza naye.
Mhe. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Zakhem.
Msomaji wangu ni dhari na ni vyema ukatambua kuwa baadhi ya wanadamu wanakupenda pale ambapo kuna kitu wanakitaka kwako na kama hauna kiukweli wanakukimbia.
Msomaji wa blog hii ni BWANA YESU pekee ndiye ambaye hawezi kukuacha atakuwa nawe mpaka mwishoi wa dahari,marafiki watakukimbia,ndugu,jamaa na hata wale ambao ni wa karibu nawe watakusaliti eti kwa sababi kile walichotegemea kupata kwako hawakioni tena kuwa makini mtegemee MUNGU pekee na wala sio wanadamu maana hata maandiko matakatifu yanasema amelaaniwa yule amtegemeaye mwanadamu.
 Mhe.John Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Zakhem jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha na kuwasalimia wakazi wa Dar es Salaam.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwatambulisha viongozi mbali mbali waliomsindikiza mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya mikutano vya Mbagala Zakheem.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za tumba pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye kwenye jukwaa la bendi ya TOT mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuhutubia  wakazi wa jiji la Dar es Salaam.




Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano wa Mhe. John Magufuli katika viwanja vya Zakhem.
picha kutoka michuzi blogspot.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni