YESU NI JIBU

Jumamosi, 25 Julai 2015

HATIMAYE RAIS OBAMA NA MWENZAKE UHURU KENYATTA WAMEFUNGUA KONGAMANO LA SITA LA KIMATAIFA KUHUSU UJASIRIAMALI KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NAIROBI.


 Hatimaye naibu wa rais wa Kenya William Ruto amefanikiwa kusalimiana na rais wa Marekani Barrack Obama baada ya kukosekana hapo jana katika ujumbe uliomkaribisha rais huyo alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. William Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC mjini the Hague.
Ikulu ya Nairobi kenya
 Ikulu
Mkutano wa kibiashara kati ya mataifa ya kenya na Marekani umeanza katika ikulu ya rais nchini Kenya.Rais Barrack Obama na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanawaongoza wajumbe kutoka mataifa hayo mawili katika mkutano huo.Swala la ugaidi ni miongoni mwa maswala tata yanayotarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho.
Rais ‪Obama pia anatarajiwa kutia sahihi ya mikataba ya kibiashara na mwenyeji wake rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi
Ruto
Rais Barrack Obama kukutana na makamu wa rais wa kenya William Ruto ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya ICC katika mazungumzo ya kibiashara kati ya Kenya na Marekani yatakayoandaliwa katika ikulu ya rais.
13.50pm:Rais Obama akiweka mauaObama
Rais Barrack Obama akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi

Memorial Park


Rais Obama na Uhuru Kenyatta wawasili katika eneo la shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi.Baadhi ya barabara katika jiji la Nairobi zimebakia kuwa mahame

 
 
Manusura 1998,
Raia Walionusurika shambulizi la 1998 kenya wabeba mabango wakidai kwamba hawakufidiwa.Wanamtaka rais Obama kutowatupa na badala yake kuangalia maslahi yao.

Wachezaji densi Nairobi
Wachezaji densi ya kimasai wakisubiri kumtumbuiza rais Barrack Obama aliyetarajiwa kuwatembelea katikati ya jiji la Nairobi

 
M-kopa M-kopa
Rais Obama kwa sasa ametembelea maonyesho ya uvumbuzi jijini Nairobi ambapo alikutana na June Muli afisa anayesimamia maslahi ya wateja M-Kopa ambao hutoa huduma ya kawi ya jua ya 'pay as you go' katika makaazi.
 
Obama-uhuru Memorial Park
Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobi
Obama na Uhuru
Obama amaliza hotuba yake
BBC hewani moja kwa moja
Runinga ya BBC inapeperusha moja kwa moja kongamano hilo hewa
Obama
Kenya inaongoza katika teknolojia za kibiashara.Kwa mfano utumizi wa Mpesa-ni vyema kwamba teknolojia hiyo ilianza hapa Kenya
Obama 'Tutazindua mfuko wa kudhamini biashara zinazoanzishwa na wanawake
Kina mama ndio injini ya maendeleo barani Afrika.
Vituo vitatu vitafunguliwa Mali,Kenya na Zambia barani Afrika ili kuwasaidia wanawake wajasiriamali
Rais Obama
Rais Obama awasalimia wakenya kwa neno 'niaje' na
Hawayuni na kusema kuwa familia yake inatoka nchini kenya.
Lengo la mkutano huu aliouzindua miaka mitano iliopita mjini Washington ni kuwapiga jeki wafanyibiashara duniani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na ufisadi ili biashara kushamiri.
Kenya ilikumbwa na chanagamoto chungu nzima ikiwemo majanga lakini imesimama imara na kusonga mbele.
Bara la Afrika haliwezi kutegemea mataifa ya magharibi .
Taifa la kenya ni chimbuko la makabila tofauti.
Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta Ges tweet
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa tayari umewasili katika eneo la mkutano wa wajisiriamali unaotarajiwa kufunguliwa na raia wa marekani Barrack Obama
Waandishi habari Waandishi
Waandishi wa habari wakijiandaa kuliangazia kongamano la kibiashara la wajasiriamali katika eneo la Gigiri jini Nairobi.
Vifaa vya waandishi hao vimepekuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.
Ndege za kijeshi
Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kuzunguka katika anga ya jiji la Nairobi kuimarisha usalama.

Barabara za Jijini Nairobi:
Barabara nyingi za mji wa Nairobi zimeonekana kuwa bila watu na magari kufuatia kuwasili kwa rais Obama.Mapema leo maafisa wa polisi walionekana katika barabara zinazoelekea katika eneo la Gigiri ambapo rais Obama atafungua rasmi kongamano la kibiashara.
Obama na familia yake Sara Obama,Barrack Obama na Daktari Auma
Mama Sarah Obama,Rais Obama na dadaake Daktari Auma Obama wakijumuika katika chakula cha jioni katika hoteli moja jijini Nairobi.
 Chanzo ni BBC.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni