YESU NI JIBU

Ijumaa, 31 Julai 2015

UNGANA NA MTUMISHI WA MUNGU PETER LUKUTA KATKA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUMALIZA MAOMBI YA SIKU 120 ZA KUIOMBEA TANZANIA

Nina mengi ya kusema lakini nasema machache tu Kwa wale wale wafwatiliaji waaminifu wa Post zangu bila shaka watakumbuka vuzuri kwa habari ya yale ambayo Mungu alisema nami kuhusu Tanzania na nikaweka Share humu fb lakini wengi walinipinga sana hata baadhi ya watumishi wakapinga sana wakakejeli wengine wakasema Kuwa natafuta umaarufu ijapokuwa pia kutafuta umaarufu si jambo baya maana Mungu aliahidi kuyakuuza majina ya watu wake na maandiko yananiambia habari Yesu zilienea kwenye miji yote ya kando kando si hilo tu bali Yesu ametutuma tuhubiri Ulimwenguni kote hii inamaana Ulimwengu woote umtambue yeye kupitia sisi hivyo umaarufu ni mapango wa Mungu kabisa acha watumishi wawe maarufu kusudi injili iendelee hamkumbuki hata yale pepo alisema Paulo tunamjua na Yesu tunamfamu hii inamaana watumishi ni maarufu kuzimu inawatambua. Ok tuyaache hayo tuendelee na kusudi la ujumbe wangu
Baada ya watu kupinga yale ambayo Mungu alisema nami hatimaye miezi michache baadaye yakaanza kuonekana kwa kishindo na yalipoonekana wazi kabisa ndipo Mungu akaniambia tena Kuwa niwakumbushe watu kuwa Mungu alisema mkapinga sasa yanatokeae. Kwa kweli wale wapinzani sikuwaona tena kwenye Post ya pili sijui walijificha wapi. Na mara hii ya pili Mungu aliagiza tufanyeje mfungo wa siku 120 ambao tulianza Tarehe 1March hadi na kuhitimisha Tarehe 28 July kwa kweli maombi haya yamekuwa na mwitikio mzuri na mpenyo mzuri na hata huduma zote nalizozifanya mikoa ambayo nimetembelea yote nalifanya nikawa kwenye mfungo huu na hata siku ya Arusi yetu mimi na mke wangu Vailethy Peter ilinikuta kwenye mfungo na nikawa mwaminifu hadi jioni ndipo nikala kwenye sherehe.
SHUKRANI ZA PEKEE
Kwanza kwa Mungu na pili kwao wote ambao wamekuwa waaminifu watumishi wa Mungu ambao tumekuwa pamoja siku zote kwenye Group letu la WhatsApp la MFUNGO WA SIKU 120 nawapongeza watanzania wote kutoka nchi mbali mbali duniani ambao mliitikia mwito huu na kweli mlitutia moyo sana pia wachungaji ambao mliitisha maombi haya kwenye makanisa yenu najua si kwa uwezo wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu tu baada ya siku zote hizi sasa natangaza ramsi kwamba Mfungo huo umekwisha

Sasa lile Group letu la WhatsApp la Maombi haya litageuka kuwa Group la maombi na ukombozi wa watu wa Mungu
Lakini hii isiwe mwisho wa kufunga bali kufunga na kuomba kuwe ni destuli yenu kama ilivyo kwangu tutaeendelea na harakati zetu za uamsho wa kanisa la Tanzania
Yapo mengi ya kufahamu juu ya hili bali kwa leo naomba kuishia hapa pia karibu kwenye Group zetu mimi na mke wangu MLIMA WA UAMSHO kwenye telegram na FUNGUO ZA UFALME pamoja na KISIMA CHA UTAKASO ukitaka tukuunganishe kwenye Group hizi Tutumieni Masage Kwenye WhatsApp No 0767 503054 na Telegram  0767 503054 tutakuunganisha.
SIMAMA KISHUJAA AMINI UNAWEZA FANYA UTASHINDA


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni