YESU NI JIBU

Jumanne, 14 Julai 2015

SOMO JUU YA ROHO MTAKATIFU KATIKA SEMINA AMBAYO IMEFANYIKA KATIKA KANISA LA TAG SAYUNI MSAKUZI JIJINI DAR ES SALAAM.

Somo la Roho mtakatifu ambalo limefundishwa na mtumishi wa Mungu mchungaji Peter Miagie kutoka Lengijave Arusha katika kanisa la T.A.G Sayuni Msakuzi linaloongozwa na mchungaji Editor Sylvester Kajuna jijini Dar es salaam.
Katika somo hilo ameelezea juu ya Roho mtakatifu kuwa ni nafsi ya tatu ya Mungu na ni muhimu sana katika maisha ya kila mkristo maana anafanya kazi mbalimbali ndani ya maisha ya mwamini na ndani ya kanisa kwa ujumla.
MCHUNGAJI PETER MIAGIE AKIWAOMBEA WAUMINI AMBAO WAMEHUDHURIA KATIKA SEMINA TAG MSAKUZI.
Kuna kazi mbalimbali ambazo Roho Mtakatifu hutenda kwa kanisa na kwa mwamini mmoja mmoja,pia ana majina ambayo mara nyingi hutumika.
1.Roho wa Kristo ,umoja na uhusiano wa utatu mtakatifu.

2.Roho wa hukumu na kuchoma
Roho wa haki,sheria na taratibu ambapo huondoa dhambi maana kwa hali ya kawaida hakuna mwanadamu ambaye anamfahamu mwenzake ila Mungu pekee anafahamu na matendo ya kila mwanadamu chini ya jua.
3.Roho wa neema na maombezi.
Hana mipaka na hawezi kuwekewa maana yeye yupo popote,na ndiyo maana hata kama mtu yupo mbali anweza kuombewa na kupokea uponyaji.
4.Roho wa hekima na ufunuo
Yeye huamua kwa haki na kila mwamini ambaye yupo tayari kumtegemea humsaidia kuamua maamuzi mengi kwa hekima.mfano Mfalme Suleimani aliweza kuamua kesi ambayo ilikuwa ngumu sana kwa kutumia hekima ambayo aliomba kwa Mungu kabla.
5. Roho wa baba yenu.
kuna uhusiano wa karibu sana ndiyo maana mara nyingi wakati wa maombi na maombezi huytajwa Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo.
6.Roho wa kweli.
Ni nafsi ya tatu ya Mungu anafahamu yote katika maisha ya kila siku ya mwamini.
7Ni Roho mtakatifu
Ni tabia yake utakatifu hivyo imetupasa waumini kuwa watakatifu katika maisha ya kila siku
Zaburi 143:10.
8.Roho wa Uzima
Ni kazi yake ROho mtakatifu kuwaombea watakatifu kutoka katika sheria ya dhambi
kolosai 1:13


warumi8:2






 Maombi na maombezi yakiendelea baada ya neno ,waumini wengi walifika mbele kuombewa nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya kanisa la TAG Sayuni Msakuzi


 Waumini ambao walihudhuria semina wakiwa katika hali ya kuabudiu huku maombi yakiendelea.



Mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG sayuni akiwaombea waumini katika semina ambayo imeendeshwa na mchungaji Peter Miagie kutoka kanisa la TAG Lengijave Arusha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni