YESU NI JIBU

Alhamisi, 23 Julai 2015

NGUVU YA MLINZI NI MACHO YAKE,UNGANA NA MTUMISHI WA MUNGU PETER LUKUTA KATIKA SOMO HILI


Yesu alitoa mfano mmoja akasema Mtu mmoja alipanda mbegu njema shambani mwake lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magumu MATHAYO 13:24-28.
Mwana wa Mungu kuna mambo mengi ya kujifunza hapa lakini nataka leo tuangalie moja tu la nguvu ya macho maandiko Yesu alisema pia kuwa macho ndiyo taa ya Mwili sawa kabisa ni kweli macho ndiyo taa ya Mwili Neno linasema kwamba Mtu aliyepanda mbegu njema shambani mwake sasa hili neno mtu linamaanisha ni mmoja lakini alikuwa na wafanyakazi wengi ambao walimlimia shamba lake na kupanda mbegu njema na hao watu ndiyo walikuwa walinzi wa lile shamba. Sasa basi pamoja na kwamba haijawekwa wazi kuwa walikuwa wangapi lakini lakini kutokana na sentensi inayotumika kuelezea tukio hilo inaonyesha wazi kwamba walikuwa si chini ya watu kumi ndiyo maana ikaandikwa WATU WALIPOLALA mimi naamini Kama wangepungua kumi ingekuwa rahisi kuandikwa watu watatu au watu watano au watu tisa ingekuwa rahisi kuandikwa watu kumi. Lakini siyo rahisi kuandikwa watu kumi na tano no hiyo ingekuwa shughuli ya ziada mimi naamini ilikuwa ni zaidi ya kumi na kuendelea. Pamoja na wingi wao na umahiri wao wa kuchapa kazi ya bosi wao lakini bado hawakujua nguvu zao usalama wao kuwa upo katika macho yao akili zao ziliwadanganya kuwa usalama wa shamba lao upo kwenye uwepo wao wa wao kutokaa mbali na eneo lile waliamini kuwa wakiwa eneo lile hakuna kibaya kinachoweza kutokea waliamini uwepo wao utamtisha adui asiweze kusogea karibu na eneo lile. Lakini kwa bahati mbaya adui yao Alikuwa na akili sana alikuwa anajua kuwa nguvu zao wao Kama walinzi haipo kwenye silaha wala nguvu walizonazo bali nguvu zao zimo katika macho yao, Unajua Mwana wa Mungu ni kwamba hawa watu walikuwa na ajira mbili mchana kulima na usiku kulinda hivyo ni wazi kwamba walikuwa na mishahara miwili yani mshahara wa kulima na mshahara wa kulinda. Ajira yao hii ni sawa na ajira ya kanisa kulima ni kutumika kwa bidii katika kuwaleta watu kwa Yesu na kulinda ni kuwa macho wakati wote katika kuwaleta watu wachanga kiroho kusudi sije wakavamiwa na mafundisho ya uongo na kutolewa Nje ya njia sahihi na ya kweli hivyo kila mtumishi anajira ya kuwavuta watu kwa Yesu pamoja na kuhakikisha anawalinda kwa maombi na mafundisho ya kuwajenga kusudi wasirudi nyuma Kama mimi ninavyofanya kwenye Group zangu zote za Whtsapp ndiyo maana nikawakataza watu kula chakula cha kusheherekea sikukuu ya Idd mubarck kwasababu ni ibada ya miungu ni sikukuu ya miungu na kuna madhara makubwa kwa mkristo aliyeokoka kula chakula kilichotolewa sadaka kwa miungu =HESABU 25:1-4 Walafi na vipofu wa kiroho wanatumia maandiko vibaya kwaajili ya kuhalalisha kula chakula cha miungu lakini nikutokana na upofu wa kiroho pia nikutokana na ulafi tu uleule uliyomponza Esau akauza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwaajili ya chakula kimoja kitu ambacho Mungu anakiita ni uasherati =WAEBRANIA 12:16. Hii inamaanisha kwamba kula chakula kinachokuvunjia uhusiano wako na Mungu ni hakuna tofauti na vijana wanaochukua makahaba na kwendanao Guest kufanya Uasherati. Najua kuna wengine nimewakwaza lakini jitahidini tu kunipenda hata hata kulazimisha kusudi roho zenu ziponywe na mafundisho yangu ya matengenezo. Sasa tunaendelea ni kwamba wale walinzi walikuwa wengi lakini hakujua anachokiogopa adui yao hivyo walipomwona adui anakatiza walinyanyua silaha zao kusudi aogope lakini adui yule macho yake hatakuwa yanatazamia zile silaha no bali macho ya adui yalikuwa yanatazama macho yao tu adui aliogopa macho yao tu lakini walinzi hawa hawakujua ni sawa na Wakristo wengi wasivyojua kuwa Shetani haogopi silaha zao za jina la Yesu tu no bali Shetani anaogopa macho yao maana nguvu ya silaha ipo kwenye macho ndiyo maana wameshindwa vita nyingi pamoja na kulitaja jina la Yesu Sikiliza mwana wa Mungu Wote waliyoshindwa si kwamba hawakuwa na silaha ya Jina la Yesu no walikuwanayo lakini walifumba macho NGUVU YA MACHO Yesu alisema Watu walipolala angalia vizuri hili neno WATU maana yake ni wengi na hawa wengi wote walilala Usingizi maana yake walifumba na macho maana huwezi kulala bila kufumba macho. ok watu walipolala akaja adui. Angalia tena hii sentensi inasema AKAJA ADUI siyo WAKAJA MAADUI no bali ni AKAJA ADUI maana yake alikuwa mmoja tu yani adui amekuja mmoja tu lakini waliyolala walikuwa weengi wengi na akawashinda kwa kufanikiwa kupanda magugu katikati ya shamba kisha akaondoka akaendazake. Wao walipoamka asubuhi hawakujua kuwa adui alikuja usiku na kuwapandia magugu sasa wao waliendelea na kuwekea mbolea pamoja na kumwagilia maji ili mazao yakue lakini kipindi wanamwagilia mazao hayo hawakujua kuwa wanamwagilia na magugu hivyo ni sawa na lile somo alilofundisha Mtumishi Vailethy Peter akasema Magugu anayapanda Shetani lakini Mkuuzaji ayeyakuuza ni mwenye shamba yani magugu anakupandia shetani lakini kukuuza unayakuuza mwenyewe. Ni kweli Shetani huwa anapanda tu mbegu ya magugu ya mafarakano kwenye ndoa lakini wakuuzaji wa hiyo mbegu ni wanandoa wenyewe kwa kuendeleza mafarakano vinyongo kuchukiana hiyo yote hutokana na kukosa macho ya kuona kuwa adui hapa siyo mke w siyo Mume wangu bali adui yetu hapa ni Shetani. Watu wengi wanashindwa kwasababu hawamwoni Shetani wao wanaonana wenyewe wenyewe ndiyo maadui na Siku zote haiwezekani kushinda vita kabla ya kumjua adui na kumwona mbinu zake. Silaha haisadii mahali ambapo macho yamefumba silaha kupita macho kwasababu macho ndiyo yanamwonyesha mlinzi mahali sahihi pakupiga huwezi kupigana vita huku umefumba macho utauawa hata Nchi zote haziajiri vipofu jeshini kwasababu kipofu haoni pakupiga ndivyo ilivyo watu wa Mungu leo hawajui pakupiga kwasabu wamefumba macho wamelala na hata wakijaribu kupigana wanapigia wao kwa wao shetani wanamwacha pembeni kwa sababu hawaoni kibaya zaidi hata nyakati baadhi ya Watumishi nao hawaoni pamoja na kujipachika majina Makubwa kwa ajili ya kuwateka watu kisaikoloji lakini hawaoni wamebakia kuonyesha shoo tu Kama kaburini flani hivi kakufurahisha macho na masikio ya watu. Kwasababu nao wamelala hawana. Adui anajua nguvu za Macho na ndiyo maana haji kwa mtu aliyemacho mtu ambaye yuko macho kwenye utakatifu kwenye utoaji kwenye maombi kwenye kufunga kwenye kufanya kazi ya Mungu kwa mali zao watu hawa ambao wako macho Shetani hawasogelei watu ambao Mungu akisema wanajua huyu ni Mungu wanatii na Shetani akija kwa njia yoyote wanajua huyu ni Shetani hapa hatumkubalii kupita kirahisi tumzuie, wanapatana na kumzuia Shetani wanashinda lakini watu ambao wamelala shetani atawagalagaza atawapepeta Kama ngano atazivunja ndoa zao atavunja undugu wao atavuruga huduma zao atawaweza kwa kishindo kwasababu wamelala hawataki Kuamka hawataki kusameheana mke hataki kumnyenyekea mumewe hataki kumtii mume hataki kumpenda mkewe hampi huduma hata mke akichukua pesa kununulia malapa tu lazima iwe kesi mke akienda kujinunulia vitu vidogo vidogo tu anasimangwa anaambiwa anatumia pesa vibaya yani mke hana uhuru na mali za mumewe mtu wajinsi hii nikipofu haoni na kamwe hawezi kuvishinda vita vya kiroho kadhalika mke mwenye kiburi hawezi kushinda vita inayomkabili. Pia na Mtu mwingine yes ambaye amelala kamwe hawezi kushinda vita walokole wengi wamevamiwa na roho za ajabu ajabu kutoka Kuzimu kutokana na kutokuwa tayari kutii ili kuwa na macho. Usisahau kwamba adui mmoja tu anaweza kuwaangamiza Wote iwe kanisa au familia familia hata taifa indepo tu watalala Usingizi. Yapo mengi ya kufahamu juu ya hili lakini kwa leo naishia hapa Kwa Ushauri Na Maswali Nitumie Masage Kwenye Whtsapp yangu 0767 503054

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni