ASKOFU SYLVESTER GAMANYWA,
Nafasi ya kanisa la Tanzania katika
changamoto zinazolikabili taifa ambazo ni ya changamoto za kiuchumi,kijaami na
kisiasa.
askofu mkuu wa WAPO Mission Internatinal Slyvester Gamanywa akizungumza katika studio za TIT Dar es salaam.
Kanisa la Tanzania nafasi yake ni ipi
na mchango wake ni ulipi hizo ndiyo agenda na kuanzia tarehe 31 Ijumaa na 1 jumamosi ukumbi wa mwalimu julias
kambarere
Aidha askofu Gamanywa alisema kuwa maaskofu,wachungaji,mitume,manabii
wanaalikwa kuhudhuria na wacha Mungu ambao wana taaluma mbalimbali ambao zitasaidia
kanisa kusimama katika nafasi yake.
Aliongeza kuwa Roho mtakatifu
anazungumza na watumishi wa Mungu katika nafasi mbalimbali na katika jumbe
mbalimbali ambazo yeye anataka taifa lisikie.
Na Katika mkutano huo watumishi
watapitia jumbe mbalimbali ambazo zilitolewa na watumishi mbalimbali na
kinachotakiwa ni kutubu tu na kugeuka na kufanya kile ambacho Mungu yeye
anataka maana
yeye sio wa malumbano wala sio
maandamano.
Hata hivyo alisema kuwa Kadi kwa wale
ambao watahudhuria katika kongamano hilo zimekabidhiwa kwa viongozi wa kanisa
na madhehebu mbalimbali na pia mtu .
Kiashirio cha kutoweka kwa amani
katika taifa la Tanzania vimeanza kuonekana na kiukweli hakuna amani kuna
utulivu ndani ya nchi.
Hata hivyo askofu Gamanywa hakuchelea
kuelezea nini kinachosababisha haya yote ambapo alisema kuna watu wanaonufaika
na mazingira ya vita na fujo zinazotokea na wao wanaochangia na wapo ndani na
nje ya nchi.
Alisema pia vita vya kiraia na jeshi usiombe,
nchii kuingia mikononi mwa jeshi sio jambo la kuliombea,na haya nasema sio kwa
lengo la kuwatisha wananchi hapana nafahamu maana wakati wa vita vya Uganda na
Tanzania limepigana nafahamu sana tu madhara ya vita.
ASKOFU DEO LUBAMA AKIWA KATIKA STUDIO ZA TIT MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM.
Katika miaka ya hivi karibuni Mungu
amekuwa akizungumza mambo mengi kuhusu kanisa na Taifa la Tanzania.
kuanzia Mwaka 2002 Mungu alizungumza
na watumishi kuwa maaskofu,wachungaji na watumishi wake wengine,wakae pamoja
ili kuomba na kutafakari Neno lake katika
umoja
Mwaka 2008 Julai Mungu alisema yupo
karibu kuingia Tanzania.
Mwaka 2014 katika mkutano wa
madhehebu mbalimbali uliofanyika DAR es salaam,Mungu alisema kuwa endapo kanisa halitaingia katika toba na maombi,amani iliyopo itatoweka na
hali ya nchi itakuwa mbaya kuliko ile ya Somalia.
Mwaka 2015 kupitia watumishi
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi,Mungu anasema tena kanisa linahitajika kuinuka
na kuchukua nafasi yake ya katika nchi.
kwa mawasiliano
0754507230 na 0784847070
MZEE GOFREY LEMA AKIELEZEA KWA MAKINI JUU YA KIONGOZI BORA NDANI YA STUDIO ZA TIT huku askofu Gamanywa akimsikiliza kwa makini na Mhe Kaduma kulia.
Kiongozi mzuri hasubiri mambo
yaharibike ila anafanya kila jitihada kutafuta ufumbuzi mapema.
luka 19:41-43
Maneno ya manabii yanatimia maaana
Mungu amekuwa akisema juu ya Taifa la Tanzania kwa muda mrefu sana,amekuwa kama
anatubembeleza watanzania maana yeye anajua kilichopo mbele wakati sisi tunajua
ya leo tu.
Mungu anataka kuingia Tanzania
kufanya kile anachotaka kufanya na hawezi kufanya jambo bila kuwashirikisha
watumishi wake.
Amosi 3:7
Wataalamu mbalimbali wanakaribishwa na
wale wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali katika taifa hili ili wapate cha
kuwaambia wapiga kura wao
Aidha Mzee Lema alisema kuwa mkutano huo
hakuna kiingilio na litanza saa tano
kami asubuhi hadi jioni.
Hata hivyo alisema kuwa vyakula
vitakuwepo ambavyo vitauzwa kwa bei ndogo sana kutakuwepo na kadi ya
kutambulisha.
Hakukawia kuwataja wanenaji katika
mkutano huo kuwa ni
Askofu Bernard Nwaka kutoka Tanzania
na Emanuel Kure kutoka Marekani.
Hta hivyo alisema ujumbe juu ya
Tanzania kwa itampata kiongozi anayetokana na Mungu 14 Agosti 2008 ulirudiwa na Moris Cerullo 2008 Taifa hili litapata Rais ambaye ni mteule kutoka kwa Mungu.
IBRAHIMU KADUMA NDANI YA STUDIO ZA TIT.
Kauli ya mh. Ibrahim Kaduma ambaye ni
mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kingdom Leadership Network Tanzania
alisema kuwa julai 2008 unabii ulitolewa juu ya Tanzania sasa ni vyema wateule waombe kwa bidii maana
hatujui huyo mteule ni nani na unabii unapomkuja haubadiliki na anayetokana na
Mungu atatenda kwa haki.
Ndugu msomaji wetu huu ni ujumbe juu ya Tanzania na sasa unaenda kutimia wewe unachukua hatua gani na unaweza kujiuliza kuwa walengwa katika mkutano huo ni viongozi wa makanisa hasa maskofu,wachungaji na watumishi wengine,wanasiasa,wafanyabiaashara na viongozi mbalimbali wa umma na sekta binafsi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni