YESU NI JIBU

Ijumaa, 1 Mei 2015

SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO,



Nataka nikukumbushe mambo manne ya muhimu kufahamu:
1. Shetani anaweza kutumia kiti chake cha enzi kama silaha mojawapo ya kukupiga vita mtakatifu
Ufunuo 13:2,7
2. Maana ya kiti cha enzi
Kiti cha enzi maana yake ni Nafasi iliyopo katika ulimwengu wa roho na ina mamlaka juu ya maisha na mwelekeo wa maisha ya watu katika eneo
3. Kila aliyeokoka anayo nafasi na anao uhalali wa kuketi na Yesu kwenye kiti chake cha enzi
Waefeso 2:6
Waefeso 1:21
Ufunuo 5:9,10
4. Ili uwe na mamlakaya kutumia nafasi uliyopewa na Yesu ni lazima uketi
Ufunuo 3:21
Mfano: kama we mwanamke, na unafanya kazi ofisini, na pia una pia una biashara, na pia unafanya kazi kanisani.
Maana yake una nafasi nne unazotakiwa kukaa kwenye kiti. Nyumba na maeneo yake, ofisini, biashara, na kanisani.
Ukikaa kwenye kiti maeneo yote hayo unakuwa na mamlaka maeneo yote hayo.
Kumbuka huwezi kuwa na mamlaka bila kuketi
Ukiketi kwenye kiti katika kila nafasi uliyonayo unakuwa na mamlaka kila eneo.

Nakwambia shetani atapata shida sana. Kwa sababu kila akienda anakuta eneo linamilikiwa tayari.
Akienda ofisini anakuta imeuzwa, nyumbani anakuta pameuzwa, shamba limeuzwa, nk vyote vinauzwa kwa damu ya Yesu. Lakini hii inakuja baada ya kuketi
Hatua nne za kufanya ili kupambana na viti vya enzi vya shetani.
1. Hakikisha umeketi pamoja na kristo
Maana hakikisha umekubali kutumika kwa ajili ya ufalme wa Mungu
Ufunuo 3:21
Unafikiri kwa nini shetani anaogopa wakristo wengi wakae kwenye kiti cha enzi?
Ngoja nikuoneshe siri iliyoko kwenye kiti cha enzi.
Ufunuo 3:21,22
Ufunuo 4: 1-11
Pia soma
Ezekiel 10:1
Ufunuo 5:11-14
Isaya 6:1,2,3
Kwenye kiti cha enzi kuna haya yafuatayo:
* chini kuna makerubi
* juu kuna maserafi
* kimezungwa na malaika wengi sana,
* kuna Roho saba wapo pale
* kimezungukwa na upinde wa mvua
* kwenye kiti kuna umeme na sauti na ngurumo


Sasa unaweza kuelewa kwa nini shetani hztaki wakristo wakalie viti vya enzi.
Ukikubali kuketi kila kinachosemwa katika kiti cha enzi kinahusu. Kwa sababu unaketi pamoja na kristo.
2. Jifunike damu ya Yesu ikulinde, wewe pamoja na lile eneo ambalo unapambana nalo.
Mathayo 23:1,2
Kutoka 11:4,5
Mungu hakumruhusu Musa aende kwa Farao pasipo kiti.
Waebrania 11:28
Kwa imani Musa akamchinja Pasaka.
Sababu ya Musa kupaka damu kwenye nyumba zao ni:
• pigo kutoka kwa Mungu lisiwapate wao
• shetani atakapokuja na hasira asiweze kuwapiga
Unapoenda kufanya vita na kiti lazima uhakikishe umeyafunika kwa damu ya Yesu mambo yako
Hakikisha unalinda nyumba yako, imani yako, mwili wako, biashara yako, kazi yako, uhai wako, mafundisho unayopata, mzaliwa wako wa kwanza nk kufuatana na vita unayopigana.
Unaachilia ulinzi wa damu ya Yesu. Ukiachilia damu ya Yesu shetani hawezi kufanikiwa hapo maana anaifahamu damu ya Yesu.
3. Omba toba kwa ajili ya kile kilichosababisha kiti kikapata nafasi na kikapata mtu wa kukikalia na kukitumia
Ufunuo 2:12-16
Zaburi 89:3,4
Kumbuka kiti cha enzi hakiji hewani ama ni cha Mungu au cha shetani

Kiti cha enzi kinafungwa katika agano kwa lazima utubu ili kuondoa uhalali wa hicho kiti.
4. Omba Mungu ahukumu juu ya miungu inayotumia kiti hicho
Hesabu 33:4
Kutoka 12:12
Kupigwa kwa wazaliwa wa kwanza Misri Mungu alikuwa anahukumu juu ya miungu ya kimisri
Zaburi 89:14
Misingi ya kiti cha enzi cha Mungu ni:

I. Haki
II. Hukumu
Kumbuka:
- ukiwa na madhabahu peke yake

Maana yake una nguvu lakini huna mamlaka kisheria
- Ukiwa na kiti peke yake
Maana yake una mamlaka lakini hauna nguvu.

Madhabahu na kiti huenda pamoja.
Ndo maana ktk ufunuo 13:2 utaona joka yaani shetani anampa mnyama nguvu, nk
Kwanini? Shetani anajua kuna agano kwa hiyo anampa nguvu mnyama. Ndo maana ukianza kupambana na viti vya enzi utaona upande wa giza saa ingine wakitumia wanyama kama paka, nyoka nk
Hukumu
Maana yake tenganisha nipate kuadhibu
Takasa
Maana yake tenganisha nipate kutumia.
Kwa hiyo omba Mungu mwenyewe ahukumu.
Hii ni siri ya ajabu unahitaji kufahamu!

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni