Mamalaka ya hali hewa nchini (TAM) imewatahadharisha wananchi
kuchukua hatua za haraka kuondoka katika maeneo ya mabondeni kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha.
Dr Agnes Kijazi
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mamlaka hiyo Dr Agnes Kijazi
amesema mvua hizo zinazoendelea kunyesha mfululizo licha ya kuwa zitapungua
kidogo na kuwasihi wananchi kuendelea kufuatilia kwa makini taarifa
zinazotolewa na mamlaka hiyo kila siku ili waweze kupata taadhari ili kuepukana
na maafa na kuhamia maeneo ambayo ni salama.
Aidha mvua hizo zimesababisha madhara makubwa ambapo mpaka sasa
Watu nane wamepoteza maisha na mamia kukosa makazi kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam .
Hata hivyo mvua hizo zimekuwa zikinyesha mfulullizo na
kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja baadhi na kusababisha foleni kubwa ya magari jijini dare s salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni