YESU NI JIBU

Ijumaa, 1 Mei 2015

IBADA 100 ZA OPERATION VUNJA MAFUNGO ZINAZOENDESHWA NA MCHUNGAJI KATUNZI WA KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA CITY CENTRE (EAGT)JIJINI DSM ZINAENDELEA HADI MAY 30 MWAKA HUU.

Na Fidea Masunga,
 Mchungaji Florian Josephat Katunzi akihudumu madhabahuni,
Mamia na maelfu ya watu wanaendelea kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali katika ibada 100 za operation vunja mafungo zinazoendelea kufanyika katika kanisa la Eagt City Centre jijini DSM.

Akizungumza na blog hii ofisini kwake Temeke jijini DSM mchungaji florian josephat katunzi ameeleza kuwa lengo kuu la ibada hizo ni kuwafungua watu kutoka katika mafungo ya giza ,kuwaamisha na kuwaingiza katika ufalme wa MUNGU.
Aidha mch.katunzi ameeleza kuwa katika ibada hizo zinazoendelea kila kila siku za jumatano hadi jumapili zinasimamia maandiko ya biblia kutoka katika kitabu cha wakolosai 1;13 na 1yohana 3;8 ,na kusisitiza kuwa watu wahudhurie katika ibada hizo waone kuwa mungu yupo, anaponya anafungua na haina haja ya kwenda kwa waganga wa kienyeji.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika ibada hizo zilizo anza mwezi January zinatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi may  ambapo katika hitimisho la ibada hizo kutakuwa na maombi maalum ya familia na kila familia itafunguliwa na kuinuliwa kimadhabahu katika ufalme wa mungu.


 Baadhi ya waumini wakiwa kanisani wakifuatilia kwa makini neno la Mungu na maombi katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam,

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni