YESU NI JIBU

Jumamosi, 9 Mei 2015

IFAHAMU BIBLIA YAKO LEO TENA.



1.Ni mfalme yupi ambaye amemwomba Mungu juu ya hekalu kwa kusema ikiwa mbingu zimefungwa hata hakuna mvua ,kwa sababu wanadamu wamekukosea wewe Mungu ,wakiomba kwa kukabili hekaluni Mungu asikie dua zao na na kuwa samehe dhambi yao.
JIBU:mfalme Suleimani
1wafalme 8:35-40;
2 wafalme 7:12-15
 2.Lakini wale watendao yaliyo mema huja kwenye nuru, kusudi ionekane wazi kwamba matendo yao yametendeka katika nani?

Jibu: Mungu.’
Yohana 3:21
3.Kwa nini wafilisti wameamua kusema kuwa wawatume watu waende kuwakusanya mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake?
Answer: ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini mwote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
1samwel 5:11

4.Mfalme Yupi ambaye amezikwa katika makaburi ambayo amejichimbia katika mji wa Daudi na alikufa katika mwaka wa ngapi wa utawala wake.
Answer: Ni mfalme Asa aambaye alikufa katika mwaka wa 41 wa kumiliki kwake
               2nyakati 16:13-14
5.Kwa nini Mungu anamtafuta mtu wa kumwabudu katika Roho na kweli?
Answer:Kwa sababu anataka ushirika na mwanadamu ili afurahie upendo wa mwanadamu aliyemuumba kwa mfano wake na kutimiza kusudi lake la ushirika.yohana 4:23-24,Luka 1:46-47.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni