Licha ya wadau mbali mbali wakiwemo
wadau wa Mambo ya Habari,wanasiasa pamoja na wanaharakati kumtaka Rais Jakaya
Kikwete asiusaini Mswaada wa Uhalifu wa Mitandao nchini wa Mwaka
2015 Hatimaye Rais Kikwete amesaini Rasmi Mswaada huo.
Akithibitisha kusainiwa kwa Mswaada
huo na kuwa sheria rasmi Sefue wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, katibu mkuu kiongozi Ombeni amesema kuwa mswaada
ukishatoka bungeni kwenda kwa rais tayari ni sheria akisaini inayofuta ni
utekelezaji.
Aidha amesema kuwa rais ametia saini
sheria ya tisa ambayo ni sheria ya ajira kwa watu ambao sio raia,sheria ya
silaha, sheria ya marekebisho ya sheria ya risiti ghalani,sheria ya mfumo wa
malipo nchini.
Hata hivyo ameongeza kuwa sheria
nyingine ni Sheria ya marekebisho ya sheria ya tume ya ukimwi,sheria ya takwimu
,sheria ya baraza la vijana,sheria ya makosa ya kwenye mtandao na sheria ya
miamala ya kielektroniki.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni