YESU NI JIBU

Ijumaa, 1 Mei 2015

HALI BADO NI MBAYA HUKO NEPAL HUKU SERIKALI YAKE IKIOMBA MSAADA ZAIDI KUTOKA KWA MATAIFA YA KIGENI.


Mamlaka ya Nepal imeomba msaada zaidi wa helikopta kutoka kwa mataifa ya kigeni baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko baya la ardhi ambapo zaidi ya watu elfu sita waliuawa.
Serikali imesema inahitaji ndege hizo kusafirisha misaada ya dharura katika maeneo ya vijiji hususan maeneo ya milimani.
Pia ndege hizo zitasaidia kuwasafirisha majeruhi ili kupokea matibabu.
Kumekua na makabiliano miongoni mwa manusura wanaong'angania usafiri mdogo ambao unatolewa na serikali.
 Serikali pia imetaka maiti zote kuzikwa punde baada ya kutolewa ndani ya vivusi.
Waziri wa fedha wa Nepal , Ram Sharan Mahat, amesema nchi yake inahitaji dola bilioni mbili kukarabati nchi hiyo ambayo miundo msingi yake imeharibiwa vibaya.
Chanzo BBC, 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni