YESU NI JIBU

Ijumaa, 1 Mei 2015

MWANDISHI MKONGWE WA HABARI KYALOEICHI OKO KESSY AFARIKI DUNIA.



Mwandishi wa habari mkongwe Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu jijini Dar es Salaam.

Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi ,amesema leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.



Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Motomoto,Shaba,Rai, na mengineyo mengi pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali.



Hata hivyo Msengi ameeleza kuwa  marehemu ameacha watoto wawili na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Chanika nje kidogo ya jiji na mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo ambapo Marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha Rosho Kilema mkoani Kilimanjaro.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni