YESU NI JIBU

Ijumaa, 8 Mei 2015

HATIMAYE MSWAADA WA UHALIFU WA MITANDAO MWAKA 2015 UMESAINIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.


Licha ya wadau mbali mbali wakiwemo wadau wa Mambo ya Habari,wanasiasa pamoja na wanaharakati kumtaka Rais Jakaya Kikwete  asiusaini Mswaada wa Uhalifu wa Mitandao nchini wa Mwaka 2015  Hatimaye  Rais Kikwete amesaini Rasmi Mswaada huo. 
Akithibitisha kusainiwa kwa Mswaada huo na kuwa sheria Rasmi  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa leo jijini Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema Baada ya Mswaada huo kupitia sehemu mbalimbali na kuonekana hauna Tatizo lolote ndio ukamfanya Rais Kikwete kusiani Mswaada huo.
Waziri Mbarawa alisema Sheria hiyo itasaidia kupunguza makosa mbali mbali ya watu wanaofanya kwa  makusudi kwenye mtandao jambo ambalo anadai italiweka taifa salama na kuondokana na tabia iliyojijengeka kwa baadhi ya watu kuandika habari na kusambaza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.
Pamoja na hayo Waziri Mbarawa amesema kwa sasa baada ya Rais Kikwete kusaini hatua inayofuata ni kazi ya Wizara hiyo kuwaelimishwa wananchi kuijua sheria hiyo ili  kuanza kutimika Rasmi.
Aidha,waziri huyo amesema kwa wale wadau mbali mbali wa masuala ya habari na wanasiasa pamoja na wanaharakati ambao walikuwa wanaubeza mswaada huo,wanatakiwa kuwasilisha hoja zao kwenye wizara yake ili hatua zichukuliwe kwenye vipengele ambavyo wizara hiyo itaviona labda vitakuwa na utata .
vilevile akawataka watanzania kuipokea sheria hiyo kwa manufaa makubwa kutokana na uharifu wa mitandao hivi  sasa ambao ulikuwa unawasumbua.
Kusainiwa kwa msaada kunatafsiriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya habari nchini ni kama umeendelea kunyonga uhuru wa habari nchini kutokana na sheria hiyo kuwepo na vifungu kandamizi kwa watu wanaotoa taarifa kwa umma kwa njia ya mitandao.
Wadau mbali mbali wa masuala ya habari waliokutana tarehe 2 ya mwezi huu mkoani morogoro siku ya vyombo vya habari duniani walimtaka rais Kikwete kutosaini mswaada huo kwani utaiweka njia panda taifa  na wakadai uhuru wa habari unazidi wambwa msalabani kutokana na vipengele vilivyopo kwenye sheria hiyo mpya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni