Waumini wa dini ya kikristo katika
mkoa wa mtwara wameitaadharisha serikali isiwe chanzo cha kuleta mpasuko kwa
wananchi wanaowatawala kwa kulazimisha mambo yanayoweza kuleta mpasuko dhidi
yao.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya
waumini wa kanisa la Anglikana baada ya tamko la jukwaa la wakristoTanzania
kuhusu katiba inayopendekezwa, mahakama ya kadhi na hali ya usalama nchini
kusomwa katika ibada maalumu ya siku ya matawi hali iliyofanya baadhi ya
waumini kupaza sauti zao na kutaka serikali kuwa sehemu ya kusimamia amani na
si vinginevyo.
Wakizungumza na ITV baadhi ya
waumini wa kanisa hilo wameendelea kupinga mahakama ya kadhi kuingizwa kwenye
katiba ya nchi na wengine wakiizungumzia katiba pendekezwa.
Akisomesha ibada maalumu ya siku ya
matawi askofu mkuu wa dayosisi ya Newala Oscar Mnung’a ambaye pia ni makamu
mwenyekiti wa askofu mkuu wa kanisa la AngAlikana Tanzania amesema jukwaa
hilo mara kadhaa limeishauri serikali lakini matokeo yake ni haya.
Akiwa mgeni rasmi katika mkutano wa
kamati ya amani ya mkoa wa Dar es salaam uliyoshirikisha viongozi wa dini ya
kikristo na kiislamu amesema msimamo wa jukwaa la wakristo Tanzania la kuipigia
kura ya hapana katiba inayopendekezwa ni hasira zisizo kuwa na tija kwa
maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni