YESU NI JIBU

Jumatatu, 13 Aprili 2015

TANZANIANI MOJAWAPO YA NCHI AMBAZO ZITASHIRIKI MBIO ZA KIGALI MARATHON MAY 23 HADI 24.


Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotegemewa kushiriki mbio za Kigali Marathon zitakazofanyika May 23-24, ambapo nchi kadhaa zikialikwa kushiriki.
 Michuano hiyo itakuwa ni ya wazi ya kimataifa, kama yalivyo ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila mwaka nchini Tanzania huku wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali kama vile Kenya wakishiriki.
Kwa mujibu wa waandaaji, chama cha riadha nchini Rwanda (RAF), mbio hizo za Kigali pia zitakuwa na msisitizo wa kudumisha amani kupitia michezo.wakimbiaji watashindana katika mbio ndefu (kilometa 42) na half marathon (kilometa 21) kwa upande wa wanawake na wanaume. Mbio hizo zitaanza uwanja wa Amahoro.
Wanariadha wengi kwa sasa wapo katika matayarisho na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Olimpiki yatakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni