YESU NI JIBU

Jumamosi, 18 Aprili 2015

HALI IVYOKUWA NYUMBANI KWA ASKOFU GWAJIMA MAENEO YA SALASALA JIJINI DAR ES SALAAM.

Wakati taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.

 Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
  Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote nyumbani kwa askofu Gwajima.
 Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.
Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano. 
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi huyo afikie kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu.
Mawakili wa askofu  Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
 Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba ya askofu wao.
Waumini wa kanisa la Ufufio na Uzima  wakielekea nyumbani kwa askofu wao  mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.

  Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo nyumbani kwake.

  Gari la polisi likiondoka katika eneo la nyumba ya askofu Gwajima.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni