YESU NI JIBU

Jumamosi, 25 Aprili 2015

IFAHAMU BIBLIA YAKO KUPITIA AMANINAFURAHA.BLOGSPOT.COM.



1.Karama ya kupambanua Roho inatolewa kwa lengo Gani?
1.  kutambua chanzo cha miujiza ,ishara na maajabu matendo 8:4-13
2.  Kutambua mawakala wa ibilisi matendo 13:6-12
3.  Kutambua aina ya roho chafu zinazotenda kazi matendo 16:16-18
4.  Kutambua vyanzo vya magonjwa na udhaifu katika miili na nafsi za watu mathayo 12:22-23
5.  Kutambua mafundisho potofu au ya uongo waebrania 1:1-2; 1thethalonike 4:13-17
2.Daudi na Jonathani walikuwa marafiki ni kitu (siri)gani kilichosababisha urafiki wao udumu toa sababu  sababu nne ama siri nne.
1.  mwambatano ulianzia katika roho zao.
2.  upendo wa kweli kati yao(1sam 18:1)
3.  utayari wa kila mmojaa wao kuwa mwaminifu katika patano la urafiki wao(1sam18:3)
4.  upendo wenye msukumo wa kutoa na kujitoa kwa hiari kila mtu kwa mwenzie(1sam18:4)

3.Ni watoto wangapi wa mfalme Sauli waliuwawa na wafilisti katika mlima Gilboa
Jibu;Ni Yonathani,Abinadabu na Malkishua
1Nyakati 10:1-2
4.mfalme Sauli aliuwawa na nani?
Alijiua mwenyewe
1Nyakati 10:4-6
5.Ni mtu yupi alikuwa anatumia uchawi na watu wengi walimogopa sana na yeye kusema kuwa ni mtu mkubwa?
Simoni
matendo 8:9-13
6.Roho mtakatifu anatusaidia katika sehemu mbalimbali ama nyingi ila katika suala la maombi hutusaidia kufanya nini na katika biblia ibapatikana wapi?
Hutusaidia katika udhaifu wetu
Warumi 8:26-27
7. Ni nani alifundisha neno la Mungu kwa nguvu sana na kuwaonya watu kutenda mabaya wapinge Roho Mtakatifu badala yake walimpiga kwa mawe hadi kufa.
Stefano
matendo 7:51-60


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni