YESU NI JIBU

Jumanne, 14 Aprili 2015

SHANGWE ZA WANAAMANI


Ni jumapili ya tarehe 12 april 2015 ni siku ya  kipekee ambayo rapper wa muziki wa  injili maarufu kwa jina la Rungu la Yesu ametangaza hadharani na kumvisha pete ya uchumba  bi Nuru Samson katika kanisa la Dar es salaam Calvary Tample(DCT) lilopo Tabata shule jijini Dar es Salaam linaloongozwa na kusimamiwa na mchungaji kiongozi RON swai ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God.
Hata hivyo ndoa yao inatarajiwa kufungwa tarehe 25 July Mwaka Huu.
 sasa kijana kitu gani kama alama unayoweka kuwa huyu ni mchumba wako. 







 Katikati mchungaji kiongozi wa kanisa la DCT akiwa na wachumba bi Nuru Samson na Rungu la Yesu kabla ya kuvishana pete.
 Rungu la Yesu akiwa na Mc Lawrence Mwantimwa mara baada ya kutangaza uchumba.
 Waumini wakifuatilia kwa makini zoezi za Rungu la Yesu Kumvisha pete Bi Nuru Samson ndani ya kanisa hilo la DCT.
Aidha Rungu la Yesu ameandika katika mtandao wake wa kijamii yaani faceboo kuwa Ashukuriwe MUNGU ambaye hujibu maombi kila wakati pia hutuwazia mema kila wakati....asante YESU kwakunipa Mdada Flani hivi Amazing ni kama naota flani hivi lkn ndio imekuwa....nimalize kwa kusema nakupenda sana mke wangu mtarajiwa Nuru George wa Rungu LA Yesu... YESU PAMOJA NASI TUTASHINDA....YOM-DAIMA.hivyo ndivyo alivyosema.
Picha na YOM,

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni