YESU NI JIBU

Jumapili, 19 Aprili 2015

KUTANA MTUMISHI WA MUNGU MWALIMU VALENCE VICENT,WA HUDUMA YA NURU YANG'AA GIZANI KATIKA SOMO LA ROHO YA UNYONGE (INFERIORITY SPIRIT):

Roho ya unyonge imekuwa ikiwatesa watu mbalimbali katika maisha yao,imekuwa ikiwasumbua watumishi ,wafanyakazi wa ndani na hata viongozi wa siasa ,inakuonesha pia Adui yako aliyeko mbele yako jinsi alivyo kuwa na mwenye nguvu kuliko wewe.
2 samweli 33
Unaona Sauli anamwambia Daudi kuwa huwezi hata kidogo  kupambana na Goliathi mfilisti na wewe unaweza ukakaa na marafiki zako ambao wana elimu kubwa kuliko wewe  na roho ya unyonge inakukatisha tamaa kuwa huwezi kukaa wala kuzungumza na watu hao maana huna elimu kama yao.
Roho ya unyonge inamwonesha mtu historia ya maisha yake na ya familia yake,kuwa huwezi maana familia yako ni maskini sana huwezi na kukaa ama kuishi na watu wengine wenye uwezo ni vigumu.
Roho hiyo inafanya historia ya maisha yako ikutangulie na kuona kwamba hauwezi kama ulishafanya kosa ama dhambi ndani ya kusanyiko na hata kama hakuna mtu aliyekuona ama kushuhudia roho hiyo inakukwamisha na kukufanya ushindwe hata kumtumikia Mungu.
Waamuzi 6:11-15
Roho ya unyonge ilimshika hata Gideoni na kuona kuwa hawezi maana familia yake ni maskini sana kuliko familia nyingine.
Ni roho ya kukatisha sana tamaa na kukufanya kushindwa,kufanya kile ambacho kitakusaidia hivyo nivyema  kusimama na kukemea na kuacha kabisa maana imekuwa ikiwakwamisha wengi.
Biblia inasema kuwa kweli yenu iwe kweli,ndiyo na iwe ndiyo na  hapana iwe hapana usiangalie roho ya unyonge maana itakukatisha tamaa na kukukwamisha,maana kuna baadhi ya watu hata wamekufa bila kufanya kazi ya Mungu na badala yake wamekufa wakiwa na mambo ya kimungu bila kutumia hata kidogo.
Hata wengine wameshindwa kufanya biashara kutokana na kuwa na  roho hiyo,ila kila jambo ambalo unataka kufanya ni vyema kumshirikisha Mungu na hapo unaendelea na kazi yako maana ukimshirikisha Mungu yeye anaongeza mara dufu.
Na hata Mungu amezungumza na Yeremia na akakataa na kudai kuwa yeye ni mtoto hawezi kumtumikia Mungu.
Hakuna mwanadamu ambaye amekamilika ,mwandamu ni mwanadamu tu ila anakamilishwa na Mungu kupitia jina na damu ya Yesu hivyo ni vyema kusimama na kukataa Roho ya unyonge ambaye imekuwa ikiwatesa watu wengi hata washirika .
Je wewe unamaoni gani ama nawe unakandamizwa na roho ya unyonge ambayo inaambatana na woga.
Itaendelea......

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni