YESU NI JIBU

Jumapili, 1 Machi 2015

MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MSIBA WA MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MAREHEMU KEPTENI JOHN KOMBA ALIYEFARIKI DUNIA JIONI YA TAREHE 28 FEBRUARI 2015.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kapteni John Komba aliyefariki dunia jioni ya tarehe 28 februari 2015 jijini Dar es salaam nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam.

 Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda yeye Mama Salma Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.

 Mama Salma Kikwete akisaini kitambu cha maombolezo.
 Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba.

Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba
  Wasanii wa TOT wakilia kwa uchungu msibani.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisalimiana na wasanii wa TOT wakati alipowasili msibani.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.
 Ndugu Fredrick Sumaye akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.
 Waziri wa ushirikiano wa kimataifa ndugu Bernad Membe akisaini kitabu cha maombolezo
 Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akihojiwa na waandishi wa habari kwenye msiba.
Picha na CCM blog na ikulu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni