Hebu
soma hapa 1Tim. 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha,
ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa
maumivu mengi. Mwisho wa kunukuu. Hapa Biblia inasema shina moja sio mawili
bali moja ni kupenda fedha, kuzipenda fedha ndio tatizo, sio fedha zenyewe,
maana fedha ni jawabu, tatizo kuzipenda. Maana wanadamu wana matatizo ya kutaka
kutupa lawama kwa mtu mwingine utamsikia mtu akisema fedha bwana ni shetani,
pesa sio shetani, pesa ni makaratasi yaliyotengenezwa. Shetani ni roho
haonekani kwa macho, pesa zinaonekana kwa macho tatizo unalo wewe unayezipenda
kufa wewe ndiyo unafungua mlango ili shetani akutumie baada ya kuona moyo wake
umeelekea kupenda fedha kuliko Mungu.
Enyi
waimbaji wa nyimbo za injili, nawaonya acheni kuzipenda pesa, ziondoeni mioyoni
mwenu muwekeni Bwana Yesu, hapa zilipokaa pesa katika moyo wako, mwache akae
Bwana Yesu vinginevyo hamtafika mbinguni, kuimba kwenyewe sio kigezo cha kwenda
mbinguni, hakuna mtu yeyote atakayeenda mbinguni kwa kuimba, kuhubiri, kutoa
pepo, kutoa sadaka, kuwa mzee wa kanisa au kuwa Mchungaji, Mtume, Nabii,
Mwalimu, Mwinjilisti bali mtakatifu pekee ndiye atakayekanyaga pale juu kwa
Baba aliye Mtakatifu. Si vinginevyo wala umaarufu wenu hautawafanya muingie
mbinguni, kwa sababu kama ni umaarufu Bwana Yesu anawashinda, kama ni
kujulikana Bwana Yesu anawashinda, tafuteni kuwa watakatifu.
Soma
hapa Ebr. 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo
utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Mwisho wa
kunukuu. Hapa vinazungumzwa vitu viwili ambayo mtu akiwa navyo atamwona Bwana,
kutafuta amani na huo utakatifu, hatuoni uimbaji wala umaarufu kuwa mtu akiwa
na vitu hivyo atamwona Bwana, sasa nyinyi waimbaji wa nyimbo za injili, hamna
amani na watu wote kwa sababu, mmechukua fedha za watu ili mkaimbe hamkwenda
kuimba pesa mmlamba kuimba hamtaki amani itatoka wapi? Mioyo ya watumishi
mbalimbali inavuja damu kwa dhuluma yenu, halafu hamajli kabisa wala hamna woga
kabisa nyie kiboko. Hofu ya Mungu hakuna kabisa kuhusu utakatifu jibu mnalo
wenyewe lakini mnajua kabisa kwamba hamkidhi vigezo vya utakatifu maana si
tunaishi na nyie tunawaona.
Jambo
lingine linalowadanganya ni umaarufu mlionao sasa ngoja niwaambie umaarufu
unaotakiwa maana hili nalo ni tatizo lingine mkijidai kuwa mnajulikana na sifa
kibao. Yer. 9:23 – 24 Bwana asema hivi, mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya
hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri
asijisifu kwa sababu ya utajiri wake bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii
ya kwamba ananifahamu mimi na kumjua ya kuwa mimi ni Bwana nitendaye wema na
hukumu na haki katika nchi, maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana.
Mwisho wa kunukuu. Kwa hiyo kama waimbaji wanataka kujulikana wajulikane kwa
Bwana kwamba wanamfahamu na kwamba na yeye anawajua, je ni kweli Bwana
anawajua? Maana yeye anasema anapendezwa na mambo ya haki katika nchi (dunia)
kwa hiyo bWana anataka haki katika vipawa vyenu vya uimbaji kitu ambacho ninyi
hamna maana mmewadhulumu watu pesa zao, mlipoliipwa hamkwenda kuimba hapo haki hakuna.
Katika
kitabu cha Wakorintho Paulo anasema hivi 2Kor. 10:17 – 18. Lakini, yeye
ajisifuye na ajisifu katika Bwana maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye
ajisifuye, bali yeye asifiwaye na Bwana.
Waimbaji
wa nyimbo za Injili, jitahidini snaa katika kuishi kwenu maisha matakatifu ili mkubaliwe na Bwana, si
vinginevyo, pia mkijitahidi sana ili mkubaliwe nay eye kama Biblia isemavyo.
Mmepewa
kipawa, kitumieni kwa haki vingienvyo mtakwenda na maji, hakuna huruma kwa
sababu huruma inajitukuza kwenye hukumu. Yakobo 2:13 Maana hukumu haina huruma
kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu. Mwisho wa kunukuu.
Lazima muwe watu wa huruma na kutoa huduma zenu popote mtakapoitwa bila ubaguzi
wa aina yoyote ile.
Itaendelea usikose sehemu ya pili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni