YESU NI JIBU

Alhamisi, 5 Machi 2015

SHAMRASHARA NA NDEREMO ZIMETAWALA KWA MUDA KANISA LA SAHARA SPORITUAL CHURCH TAG MABIBO BAADA YA KIJANA ALBERT FERDINAND KUTANGAZA UCHUMBA KWA REHEMA MYOMBE

Hongera Albert na Rehema kwa kufanya maamuzi ambayo ni mazuri ya kutangaza nia na kuvishana pete,timu nzima ya amaninafuraha inawapongeza sana na Mungu awatangulie katika majukumu yaliyoko mbele yenu ya harusi.
 
Kijana Albert akiwa na mpambe wake.
Binti Rehema kushoto akiwa na mpambe wake madhabahuni kabla ya kuvishwa pete.
Askofu wa kanisa la TAG mabibo spiritual Center akitangaza uchumba wa kijana Albert kanisani.
Rehema akimgeukia mchumba wake ambaye yupo mbele yake ,kwenye picha haonekani mpambe wake akitabasamu.


Rehema nakuvisha Pete hii iwe ni ukumbusho kwako kuwa sina mchumba mwingine zaidi yako ninakupenda na ninakuombea nawe niombeeMungu atusaidie tufikie malengo yetu la kufunga ndoa takatifu.


Hapo sasa maombi na maombezi juu ya Albert na Rehema ili Mungu awasaidie katika mikakati yao.

Sasa nimetangaza kuwa Albert na Rehema ni wachumba.

Hapo sasa zoezi la zawadi na kuwapongeza kwa maamuzi waliyofikia.


Baada ya kuvisha pete na kupewa zawadi mbalimbali kabla hawajaenda kukaaa.
Karibu kwa maoni yako.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni