YESU NI JIBU

Jumatano, 18 Machi 2015

MTUMISHI WA MUNGU WA HUDUMA YA FULL GOSPEL INTERNATIONAL MINISTRY ASKOFU ZAKARIA KAKOBE AHOJI WAKOVU WA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).



Askofu Mkuu wa huduma ya Full Gospel International Ministry Zakaria Kakobe, wakati anahubili injili kanisani kwake alisikika akisema kuwa malkia wa muziki wa injili Rose Muhando hajaokoka na anahitaji kurudi msalabani ili apate wokovu wa kweli. Akaendelea kusema uimbaji wake wa kuambatana na mastage show wanaume ambao katika kuimba kwake wao wanakuwa wanacheza huku wakizungusha kiuno hiyo ni ishara tosha inayoonyesha kuwa Rose Muhando na team yake ni wasafiri wa kwenda motoni. Kwasababu amechukua style ya kukata viuno bar na kuileta kanisani. Akiendelea na mahubiri hayo alimtaja pia Nape Nnauye, Philip Mang'ula, Makonda, Mwakyembe na Nyarandu kuwa hawajaokoka, na wanahitaji kuugeukia msalaba wa Yesu ili wapate wokovu wa kweli. Huku akionyesha kumuhoji Nape kuwa ana wake wangapi? Akiendelea na maonyo hayo amewaasa viongozi hao kuwa kama wameokoka kweli mbona hawasimami mstari wa mbele na kumtangaza Yesu bali wao wamekuwa ni wajanja wajanja tu.
Una maoni na ushauri gani juu ya mahubiri ya askofu Kakobe,


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni