Harusi moja ilitibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli
swali rahisi sana la hisibati aliloulizwa na bi harusi.
''15
ukiongeza 6 utapata nini ''?
Polisi
katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India wanasema kuwa sherehe za harusi hiyo
zilitibuka baada ya bi harusi kufoka mumewe mtarajiwa alipotoa jibu lake . ''17
''
Alikurupuka
na kuondoka jukwaani akiwa amenuna akisema hawezi kuoa mtu ambaye hakwenda
shuleni.
Juhudi
zote za jamaa na marafiki waliofika kushuhudia nikaa hiyo ziliambulia patupu.
Polisi
katika jimbo hilo la Uttar Pradesh wanasema kuwa jamaa wa bwana na bi harusi
wote walikubaliana kurejesheana zawadi zote walizokuwa wametoa kwaajili ya
wapendwa hao.
Asilimia
kubwa ya ndoa zote nchini India hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi
hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao.
Babake
bi harusi Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha
Rasoolabad aliiambia idhaa ya kihindi ya BBC kuwa mwanawe alishangaa kuwa
mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa msomi.
Mwezi
uliopita bi harusi mwengine aliolewa na mgeni katika harusi yake baada ya
Mumewe aliyekuwa amepanga kumuoa kuanguka kifaa dakika chache tu kabla ya
wawili hao kuunganishwa kuwa mume na mke .
Toa maoni yako,
Chanzo BBC,
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni