YESU NI JIBU

Jumatano, 14 Januari 2015

WATU WANAOSADIKIWA WASHIRIKINA WAMEKAMATWA KATIKA MKUTANO WA INJILI:


Wanawake watatu wanaosadikiwa kuwa ni washirikina wamekamatwa baada ya kuanguka katika mkutano wa Injili, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka kumi na tatu waliosadikiwa kuwa wakiloga madhabahu,  iliyojengwa kwa chuma, wakati Askofu wa huduma ya Hosana Life Mission Barani Afrika Efraim Mwansasu akihubiri katika eneo la Iyunga Tazara Jijini Mbeya.Baada ya kukamatwa wanawake hao ambao wote ni wakazi wa  eneo hilo wawili miongoni mwao waliamua kumpokea Yesu Kristo ili kuweza kuondokana na aibu iliyowapata.
Katika mkutano huo  watu wengi walimpokea Yesu Kristo ili kuwa bwana na mwokozi wa maisha ya  na wengine kupokea  miujiza yao wakiwemo akina mama wawili,  ambapo mmoja alijifungua mtoto wa kike baada ya kukaa miezi kumi na mbili pasipo kupata uchungu na mwingine kurudishiwa nyota yake iliyokuwa imeibiwa na mumewe kwa ajili ya kuendeshea biashara yake.
Askofu Mwansasu aliwataka Watanzania kutambua ongezeko la thamani ya Yesu Kristo kwa kuwa huleta thamani katika maisha ya mwanadamu kwa kuponya magonjwa yote pamoja na kurekebisha maisha ya mtu yaliyokuwa yamekataliwa na watu na hatimaye kuinuliwa pamoja na kurekebisha familia zao.Mbali na hayo Askofu Mwansasu aliwataka wakazi wa mkoani Mbeya kuuombea mkoa wao ili waweze kuondokana na imani potofu zinazo tokea kila kunapokucha pamoja na kuishindania imani ya kweli waliyoachiwa na Yesu Kristo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni