YESU NI JIBU

Jumapili, 4 Januari 2015

IBADA YA MAOMBI NDANI MWA MAOMBI SIKU YA TAREHE MOJA JANANUARY 2015 IMEKUWA YA BARAKA SANA MAOMBEZI YALIFANYIKA KWA KILA MTU NA KUOMBEWA KAZI YA MIKONO YAKE:

Wengi washuuhudia kupokea uponyaji na kufunguliwa kutoka katika matatizo mbalimbali za pepo wabaya na sasa wanaelezea walivyofunguliwa katika maisha yao.
Katika ibada ambazo huendeshwa na kanisa Evangelistic Assemblies of God (EAGT) City Center katika viwanja vya mwalimu Julias Kambarage Nyerer e ambayo mara nyingi siku za jumapili hutumia ukumbi wa PTA na siku za katikati ya wiki hutumia ukumbi wa Ngorongoro wengi wemeshuhudia kupokea uponyaji.
Siku ya Tarehe moja ilikuwa ni ibada ya tofauti sana hasa pale maombi na maombezi juu ya kuombbea kazi za kila mtu ambaye amewasili katika ukumbi huo na wale ambao wanasikiliza matangazo ya moja kwa moja kupitia WAPO redio FM.
Sasa endelea kufuatilia matukio kwa njia ya picha ambayo yaliendelea katika ibada hiyo,wengi walifika na vitu ambavyo wanavitumia katika kufanyia kazi zao za kila siku.

 Mchungaji Florian Katunzi akifundisha neno wakati wa ibadaa ya tarehe 1jan 2015.
 
 Wakati wa maombi na maombezi mchungaji Katunzi akiwaombea waumini waliofurika katika ukumbi wa PTA.

 wakati wa kusifu na kuabudu Rachael Katunzi ambaye ndiye mama mchungaji Katunzi akishiriki katika ibada ya sifa.

 kipindi cha maombi na maombezi mama mchungaji Rachael Katunzi.


 


 Waumini wakishiriki katika ibada ya maombi kabla ya maombezi ya kazi ya kila mmoja.
 Mtangazaji wa WAPO FM bi Angelina Lukindo akiwa na tabasamu akiwa katika viwanja vya sabasaba wakati wa ibada ambapo ibada hiyo ilitangazwa moja kwa moja na kituo hicho cha redio.








 Hapa sasa ibada maalum ya maombi na maombezi kuombea kazi ya mikono ya watu ambao watu wengi wamefika na baadhi ya vifaa vya kazi zao ambapo MUNGU alitenda mambo makuu ya ajabu sana watu wengi walifunguliwa na kuweka kuru kutoka kwa nguvu za giza.
ukiwa na uhitaji wa maombi na maombezi ama ushauri wa namna  moja ama nyingine wasiliana na mchungaji Florian Josephat Katunzi kwa namba 0718267171 ,0784367826 au 0754367826 na utainuliwa kutoka hatua moja kwenda nyingine.
ila kama unaushauri au maoni juu ya blog hii unaweza kutumia namba 0682672828 au 0779632616

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni