Ama kweli Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hawa
Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na
Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe
ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) visiwani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.
Hawa akizungumza na gazeti hili alidai kwamba Ameir
ni mume wake walifunga ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto
wanne, lakini mmoja alifariki dunia.
“ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa
wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha
mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alidai Hawa.
Alidai kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka
tisa na mwingine miaka sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa
na mwanamke aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“ Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu
niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi
nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki
anipe haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa.
Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi
yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa
akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye.
“ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini
sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka
kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.
Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa
hawakulitarajia.
“Tulivamiwa na wanawake kama wanne na wanaume
wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga
kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,”
alisema.
Alisema kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama
wa ukumbi na walifika na kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa
hatua zaidi.
wewe una maoni gani juu ya kiongozi kumtelekeza mtoto wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni