Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi sanjari na mashirika ya dini na watu binafsi wametakiwa kujitokeza na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuwakwamua na kujisikia kama watu wengine katika maisha yao.
Askofu Geofrey Masawe kulia mwenye koti jeusi akimkabidhi TV ya nchi 21 na deki mwalimu mkuu wa shule ya umoja Bwana
Abeli Ali Dimbwa na katikati ni mzee kiongozi Mzee Harrison Myombe.
Abeli Ali Dimbwa na katikati ni mzee kiongozi Mzee Harrison Myombe.
Kauli hiyo
imetolewa na Askofu wa jimbo la mashariki kaskazini ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la
TAG Mabibo Sahara askofu Geofrey Massawe wakati akikabidhi TV ya nchi 21 na
deki yake kwa mkuu wa shule ya umoja iliyopo kata ya Mabibo manispaa ya
kinondoni ambayo ina kitengo cha watoto
wenye ulemavu wa akili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwasaidia watoto hao
kujifunza.
Aidha Askofu
Massawe alisema kuwa kama kanisa wameona uhitaji wa watoto hao wa shule hiyo ya
umoja walipotembelea shule hiyo na kujionea na kusikia pia mahitaji yao na
kuona kuwa ni vyema kuwasaidia kwa baadhi ya vifaa ambavyo vitawasaidia
kujifunza maana watoto hao wanahitaji kujifunza kwa kuona wakati mwingine.
Hata hivyo
amewataka taasisi na mashirikika ya dini na yasio ya kiserikali kujitokeza kuwasaidia
watoto hao maana wanahitaji kusaidiwa ili nao waweze kupata elimu ambayo
itawasaidia kujitambua na kuweza kuishi ndani ya jamiii.
Mzee kiongozi Harrison Myombe mwenye miwani akizungumza na mkuu wa shule ya umoja BWana Abel Dimbwa huku kulia askofu Masawe akisikiliza kwa makini pamoja na watu wengine.
Akizungumza
na blog hili ofisini kwake mchungaji Oliver Massawe ambaye ni mchungaji
msaidizi wa kanisa hilo la TAG Mabibo Sahara alisema kuwa inapendeza sana kama
watu waote wenye uwezo bila kujali dini,itikadi wala rangi kujitokeza
kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa akili wanaosoma katika shule ya msingi umoja
ili nao wajisikie kama watoto wengine.
Tatizo la
watoto wenye ulemavu wa akili sio la wazazi wa watoto hao pekee hapana ni tatizo la jamii nzima
hivyo nawasihi viongozi wa dini ,viongozio wa serikali na vyama vya siasa
pamoja na asasi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia shule hiyo ili watoto hawa
wapate vifaa ambavyo vitawawezesha kuishi ndani ya jamii,alisema mchungaji
Oliva Massawe.
Aliongeza kuwa ni jukumu la kanisa kuwasaidia kimwili watu wenye
ulemavu wa aina mbalimbali,mbali na kuwasaidia kiroho inabidi kujitokeza na
kuhakikisha kusaidia kupunguza mapungufu ambayo yanaonekana katika baadhi ya
shule za watoto wenye ulemavu.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya msingi Umoja mwalimu Abeli Ali Dimbwa
amesema kuwa shule hiyo inamapungufu mengi ambapo ameendelea kuto wito kwa
wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia shule hiyo ili watoto wenye ulemavu wa
akili wanaosoma hapo kupata vifaa muhimu ambayo itawasaidia kujifunza.
Wanafunzi wenye ulemavu wa akili wakipokea zawadi ya tv ambayo itawasaidia katika masomo yao.
Ni vyema
ifahamike kuwa jukumu la kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali na
wanaoishi katika mazingira hatarishi ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha
kuwa wanasaidiwa ili nao wafikie malengo yao katika jamiii .
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni