YESU NI JIBU

Jumatatu, 19 Januari 2015

MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA EAGT CITY CENTER AMFURAHISHA MDHAMINI NA MSHAURI MKUU WA EAGT KWA KUMJENGEA NYUMBA YA KISASA:

Mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Centre Florian Josephat Katunzi amekabidhi nyumba ya kisasa aliyoijenga kwa ajili ya Mdhamini na Mshauri Mkuu wa kanisa la EAGT, ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa kanisa hilo, Mch. Anyandwile Mwakisyala,  katika eneo la Nsonyanga Mbarali Mbeya,  katika sherehe iliyoliza na kuchekesha viongozi mbalimbali waliohudhuria na wakazi wa mbeya.
Askofu Mkuu wa EATG, Asumwisye Mwaisabila.
Askofu Mkuu wa EATG, Asumwisye Mwaisabila (Wa pili kulia) akifafanua jambo fulani wakati akiangalia nyumba ya Mdhamini wa kanisa nilo, Mchungaji Anyandwile Mwakisyala  iliyojengwa na Mchungaji Florian Katunzi,katika kijiji cha Nsonyanga, wilayani Mbalali mkoani Mbeya .
Katibu Mkuu wa kanisa la EAGT, Mchungaji Brown Mwakipesile akisoma Biblia wakati wa kuiweka wakfu nyumba ya mchungaji Anyandwile Mwakislaya, ambaye ni Mshauri Mkuu na mdhamini wa kanisa hilo, akizungukwa na maaskofu wa kanisa hilo waliokuwa mashuhuda wakati wa kuiweka wakfu na kumkabidhi. Wa kwanza kushoto ni Mchungaji Florian Katunzi.
Katibu Mkuu wa kanisa la EAGT, Mchungaji Brown Mwakipesile akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wakati wa kuiweka wakfu nyumba ya mchungaji Anyandwile Mwakislaya, ambaye ni Mshauri Mkuu na mdhamini wa kanisa hilo, akizungukwa na maaskofu wa kanisa hilo waliokuwa mashuhuda wakati wa kuiweka wakfu na kumkabidhi. Wa kwanza kushoto ni Mchungaji Florian Katunzi.
 Mchungaji Anyandwile Mwakislaya, Mshauri Mkuu wa Kanisa la EAGT,  akimwombea maombi ya Baraka, Mchungaji Florian Katunzi wa kanisa hilo City Centre la jijini Dar es Salaam, huku Askofu Mkuu wa kanisa hilo Asumwisye Mwaisabila, akishuhudia tukio hilo.

 Mchungaji Florian Katunzi akimpa mkono mke wa  Mchungaji Anyandwile Mwakislaya Bi Rahabu baada ya kuombewa maombi ya baraka na mchungaji.

  Mchungaji Anyandwile Mwakislaya ambaye ni Mdhamini na Mshauri Mkuu wa kanisa la EAGT.

 Bi Rahabu mke wa  Mchungaji Anyandwile Mwakislaya.

 Mchungaji Christomo Ngowyi akinena katika kukabidhi nyumba kwa mchungaji Mwakislaya huku Katibu Mkuu wa kanisa la EAGT, Mchungaji Brown Mwakipesile akimsikiliza kwa makini.

 Mchungaji Ngowi akisalimiana na mke wa mchungaji Anyandwile Mwakislaya huku viongozi wakishuhudia.

Katibu Mkuu wa kanisa la EAGT, Mchungaji Brown Mwakipesile akifungua nyumba.

Askofu Kenneth Kasunga wa Kanda za Nyanda za Juu kusini kati mwenye suti bluu,kulia mwenye biblia ni katibu mkuu wa EAGT,wa tatu kutoka kulia ni askofu mkuu,mwenye tai ya bluu ni mchungaji Cristomo Ngowi na kushoto mwenye Kola jeupe na miwani ni mchunhaji Florian Katunzi.

Nyumba ya awali ambayo Mchungaji Mwakisyala ameitumia tangu mwaka 1969 kijijini Nsonyanga hata kufikia sasa kujengewa Nyumba nyingine ya kisasa.

Mchungaji Katunzi aliyeshika kiuno alipokuwa anaisimamia Ujenzi wa nyumba ya kisasa aliyomjengea Mchungaji Mwakisyala kabla ya kukabidhiwa tarehe 07 Januari 2015
Askofu Kenneth Kasunga wa Kanda za Nyanda za Juu kusini kati  akiongoza jopo la Maaskofu na Viongozi wa juu wa Kanisa hilo kwenye Ibada Fupi ya Shukrani baada ya ufunguzi rasmi wa Nyumba hiyo iliyojenga na Mchungaji Katunzi.
Katibu Mkuu wa kanisa la EAGT, Mchungaji Brown Mwakipesile.
 Baadhi ya Waumini wa Kanisa la EAGT Nsonyanga walioshindwa kujizuia wakati Ibada fupi ya Kukabidhiwa Nyumba Mchungaji Mwakisyala na Mchungaji Katunzi wakishangilia kwa furaha wakati ibada ilipokuwa inaendelea Kanisani hapo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni