YESU NI JIBU

Jumapili, 11 Januari 2015

IBADA MAALUM YA KUOMBEA AMANI TANZANIA:

Katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi wa madiwani ,wabungu na rais sanjari na kupigia kura katiba pendekezi viongozi mbalimbali wa dini wamekuwa wakiandaa makongamano mbalimbali ya kuombea amani katika taifa la Tanzania.
Aidha baadhi ya watumishi hawakuwa nyuma kuzungumzia juu ya suala la uchaguzi na juu ya kura ya rasimu ya katiba pendekezwa.
Hivi karibuni huduma ya House of  Prayers inayosimamiwa na kuongozwa na mchungaji Patric Kayimbi Emanuel a.k.a PKE ameandaa kongamano la maombi juu ya kuombea Tanzania ambani ambapo amejumuisha madhehebu mbalimbali.
 Watumishi wa Mungu wakiombea kitambaa ya bendera Tanzania kuwakilisha Taifa.MAOMBI HAYA YALIYOONZWA NA WATUMISHI WA MUNGU Apostle Pke PatrickKayimbi Emmanuel, Apostle Moses, Apostle Bethania Simon, Evangelist Emanuel Nicodemus NA Evangelist Azaria Kasunga,MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE .
Katika maombi hayo kabla ya kuanza watumishi wa Mungu hao wameanza kwa kumshukuru Mungu kwa ajili ya miaka kumi ya uongozi wa rais Jakaya Mrisho Kikwete,kumshukuru Mungu juu ya serikali iliyotumika chi ni ya rais Kikwete sambamaba na kumshukuru Mungu juu ya madiwani,wabunge na viongozi wa serikali za mitaa ambao wamechaguliwa.
Maombi ambayo yamefanyika ni kama yafuatayo;
  1.  kuombea uchaguzi kwa kuikabidhi mikononi mwa Mungu.
  2. kuombea uteuzi wa wajumbe kutokuwepo na upendeleo
  3. kuombea kampeni
  4. kuombeaa taasisi mbalimbali sizitumike kisiasa
  5. kila atakayeteuliwa na kuchaguliwa atokane na mapenzi ya Mungu
  6. kila atayeteuliwe apate kibali kwa wananchii.
Wakati wa kufikia ukingoni mwa maombi hayo watumishi wa mungu walisimama na kuvunja maroho ya vurugu na umwagaji wa damu,kukataa kampeni kuwa sehemu ya kuchochea chuki,kukiri kibali juu ya Tanzania Yeremia 29:7,
Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa BWANA; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani. 


Mwinjilisti Emanuel Nicodemus akiongoza maombi,
Apostle Pke PatrickKayimbi Emmanuel akifundisha neno kabla maombi na maombezi kuanza ya kuombea Tanzania.
Bishop Mak akiongoza watumishi wa Mungu kuiombea Tanzania.



Makamu askofu wa huduma ya Mighty Revival assemblies akiwaongoza watumishi wenzake kuombea Taifa la Tanzania.
Mwinjilisti Azaria Kasunga akiongoza maombi.

Apostle Moses akiongoza watumishi wa Mungu kuiombea Tanzania ndani ya House of Prayer Centre,

Apostle Bethania Simon akiongoza watumishi wa Mungu kuiombea Tanzania.


Mama mchungaji PKE akiombea watakaoteuliwa na kuchaguliwa katika uchaguzi wapate kibali kwa wananchi.


Watumishi waliohudhuria katika kongamano hilo la maombi wakiwa katika picha ya pamoja.

Apostle Mosses akiwa katika picha ya pamoja na apostle PKE mara baada ya maombi kwisha katika ukumbu wa House of Prayer.
Kutoka kulia ni apostle Mosses katikati ni mwinjilisti Azaria Kasunga na kulia ni apostle PKE.
Mwinjilisti Emanuel Nicodemus akiwa na apostle PKE.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni