YESU NI JIBU

Jumamosi, 17 Januari 2015

IFAHAMU BIBLIA YAKO,JIFUNZE NENO LA MUNGU MAANA LINAHUISHA:


1.Neno kuabudu lina maana gani?
Answer:Ni tendo linalogusa akili,hisia,nafsi na utu wa mtu na mwili pia kwa kusujudu,kuanguka kifudifudi,au uso kwa uso
mwanzo 17:3 Tendo hilo hufanywa pasipo ushawishi wa kitu ,wala si nje ya moyo wa kumtambua Mungu kuwa wa thamani  kuliko kitu chochote anayestahili kupewa ibada ya pekee na kupelekea kujitoa kwake bila unafki wala ubinafsi .
2.Kwa nini Mungu anamtafuta mtu wa kumwabudu katika Roho na kweli?
Answer:Kwa sababu anataka ushirika na mwanadamu ili afurahie upendo wa mwanadamu aliyemuumba kwa mfano wake na kutimiza kusudi lake la ushirika.yohana 4:23-24,Luka 1:46-47.
3.Karama Tisa za Roho Mtakatifu zimegawanyika katika mafungu matatu nazo ni zipi
      1.Karama za ufunuo
·       Neno la maarifa
·       Neno la hekima
·       kupambanua Roho
2.Karama za uwezo
·       imani
·       karama za kuponya
·       matendo ya miujiza
3.Karama za usemi
·       Unabii
·       Aina za lugha
·       Tafsiri za lugha
4.Kuna aina ngapi za hekima zitaje?
1.Hekima za kibinadamu ambayo wakati mwingine hujulikana kama hekima ya dunia
  mathayo 11:25,1korintho 1:20.
2.Hekima ya kishetani   ezekieli 28:17
3.Hekima ya Mungu  Daniel 2:23, 2timotheo 3:15

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni