YESU NI JIBU

Jumamosi, 3 Januari 2015

MWAKA WA 2015 WAANZA KWA NAMNA YAKE BAADA YA KIKUNDI CHA PANYA ROAD KUSABABISHA USUMBUFU KWA WANANCHI WA MAENEO MBALIMBALI YA JIJI LA DAR ES SALAAM:

Kundi linalojiita Panya Road ambalo limepigwa marufuku na jeshi la polisi limeibuka tena kisirisiri na kuanza kuwasumbua wananchi katika maendeo mbalimbali ya jiji la Da es salaam na hata kusababisha wananchi kupata usumbufu kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.

Polisi wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova.
Pamoja na vurugu hizo zote kamanda Suleiman Kova amewaondolea wananchi hofu kuwa jeshi la polisi kanda maalum limeimarisha ulinzi.

 Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Mabibo,Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundi makundi. Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzao, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo. Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar. Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa. Wateja waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.
Baada ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni