YESU NI JIBU

Alhamisi, 15 Januari 2015

AMANI SRI LANKA YAHIMIZWA NA PAPA FRANCIS


Papa Francis akizungumza katika hekalu la Buddha, Asia.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameendelea kuhimiza ujumbe wa umoja  kwa Sri Lanka kwenye misa iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mku wa nchi hiyo.

Umati mkubwa ulimiminika kwenye barabara karibu na ufuo wa bahari mjini Colombo siku ya jana kumshangilia Baba mtakatifu akiwa amebebwa na gari lake maalum. Wakati wa misa hiyo , alimtawaza mchungaji Joseph Vaz akisema kuwa utawazo huo ambao ni wa kwanza nchini Sri Lanka unaashiria umuhimu wa kuwa na amani  inayopita migawanyiko ya kidini.
Vaz alikuwa mmishonari wa karne ya 17 anayekumbukwa kwa kuifufua imani ya kikatoliki wakati waumini walikua wakiteswa na wareno wenye imani tofauti. Kesho Alhamisi Baba Francis ataelekea Ufilipino kwa ziara ya juma nzima ya eneo hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni