YESU NI JIBU

Jumatano, 9 Desemba 2015

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIM MAJALIWA ALIWAONGOZA UMATI WA WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU LA KARIAKO KUFANYA USAFI KUADHIMISHA MIAKA 54 YA UHURU.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni wanaoingia nchini.
Ametoa wito huo leo kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi


 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la  Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  kushoto  kwake ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
 Baadhi ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko hilo.

 Gari alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9, 2015. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni