Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya
rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha
uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika
katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada
ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali
ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa
kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge”
Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu
wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa
haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na
badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika.
Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa
RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali
vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.
Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya
umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi
zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika
ukiukwaji wa sheria.
Pamoja na kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Tito na Kuvunjwa kwa Bodi ya RAHACO, Rais Magufuli pia amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuanza uchunguzi wa kina mara moja kuhusiana na sakaata hilo la ukikwaji wa sheria ya manunuzi katika zabuni ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kisasa yaani "Standard Gauge".
Pamoja na kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Tito na Kuvunjwa kwa Bodi ya RAHACO, Rais Magufuli pia amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuanza uchunguzi wa kina mara moja kuhusiana na sakaata hilo la ukikwaji wa sheria ya manunuzi katika zabuni ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kisasa yaani "Standard Gauge".
Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi
ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo
ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya
treni.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
22Desemba, 2015
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni