YESU NI JIBU

Jumatano, 2 Desemba 2015

KATIKA KULINDA NA KUTUNZA AFYA YAKO ILI UWEZE KUFANYA KAZI ZAKO KWA UBORA:

Leo ni siku nyingine wapendwa wasomaji na wadau wa www.amaninafuraha.blogspot.com karibuni tujuzane kidogo juu ya afya zetu na jinsi ya kuzilinda.


Mdau wanguunaweza kujifunza mengi sana juu  aina mbalimbali za sharubati (JUICE)ambazo huwa na faida ndani ya miili yetu.
Juisi ya Machungwa.
Aina hii ya juisi mbali na kuwa na ladha nzuri lakini pia ina faida ndani ya mwili  kwani ina kirutubisho kiitwachio antioxidants.
Pia ndani ya juisi ya chungwa kuna vitamin C nyingi ambayo ni nzuri kwa afya ya ngozi,ukuaji wa mifupa pamoja na kuboresha mzunguko wa damu vizuri ndani ya mwili.
Juisi ya Nyanya
Juisi hii nayo inaumuhimimu wake ndani ya miili yetu kwani ina vitamin E ambayo ni nzuri pia kwa afya ya ngozi, lakini pia juisi hii ni nzuri sana kwa shinikizo la chini la damu lakini pia husaidia kuimarisha kinga za mwili.
Juisi ya Karoti.
Karoti ni mojawapo ya juisi bora kwa afya kutokana na kuwa na vitamin A nyingi sana pamoja na vitamin B na madini kama vile 'calcium' iron, magnesium, sodium. Hivyo virutubisho vyote ni muhimu sana kwa mwili.
Juisi ya Apple
Apple ni mojawapo ya tunda ambalo ni zuri hivyo hata juisi yake pia ni nzuri kwa afya. Juisi ya tunda hii ni nzuri kwa afya ya moyo.
Unapokunywa glasi moja ya juisi ya apple kila siku inamaana unakuwa unaimarisha afya ya moyo wako kwani husaidia kupunguza kiwango cha 'cholesterol' kwenye mishipa ya damu, lakini pia apple lina kiasi kingi cha nyuzinyuzi pamoja na vitamin C.
kwa mengi zaidi unaweza ukawasilia na Mandai kwa barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni