YESU NI JIBU

Jumatano, 9 Desemba 2015

MAADHIMISHO YA 9 DESEMBA WATANZANIA WAUNGANA NA RAIS MAGUFULI KUFANYA USAFI KATIKA UFUKWE WA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM

Maadhimisho ya miaka 54 ya  Tanzania bara yameadhimishwa kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini yakiongozwa na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambapo alishiriki kufanya usafi katika maeneo ya Ferry na kuzungumza na wavuvi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.






 

Rais  Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka taka kwenye dastibin wakati akifanya zoezi la kufanya usafi 



 Rais  Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wavuvi wa ferry huku akiwa ndani ya Mtumbwi. Rais Magufuli alizisikiliza kero zao na kuahidi kuzitatua ndani ya muda mfupi.
Rais Magufuli akifanya usafi pamoja na wavuvi wa eneo la ferry waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa na Utamaduni wa kufanya Usafi kila wakati ili kuweka mazingira katika hali nzuri. PICHA ZOTE NA IKULU


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni