YESU NI JIBU

Jumatatu, 14 Desemba 2015

LEMA AIBUKA KIDEDEA TENA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI kwa kura 68,848.


Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo - CHADEMA  katika Jimbo la Arusha, GODBLEES  LEMA ameibuka  mshindi  na  kutangazwa kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha  vyama  vitano  vya siasa, LEMA amepata kura 68 ,848  kati ya kura 104,353  zilizopigwa  akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi, PHILEMON  MOLLEL aliyepata kura  35 ,907.
Wagombea wengine  walioshiriki  katika  uchaguzi  huo  ni pamoja na NAVO  MOLLEL wa  ACT Wazalendo  aliyepata  kura  342,  ZUBERI MWINYI  wa Chama cha Wananchi -CUF-   aliyepata  kura 106 na  MAKAMA RASHIDI  wa  NRA  aliyepata  kura  43.
Kwa mujibu wa Msimamizi  wa Uchaguzi  wa Jimbo  la Arusha,  JUMA IDDY,wapiga kura walioandishwa ni 317 814, na waliojitokeza  kupiga  kura ni 105, 800.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni