YESU NI JIBU

Jumapili, 13 Desemba 2015

ATENDAYE DHAMBI NI WA IBILISI KWA KWA IBILISI HUTENDA DHAMBI TANGU MWANZO:

I YOHANA 3:8.Jina la Bwana lihimidiwe milele nataka kusema neno nawe japo kwa ufupi. Ni hivi hakuna ushirika wowote kati ya Mungu na dhambi hakuna hata kidogo haijawahi kupokea na kamwe hatowahi kutokea milele pamoja na kwamba siku za leo dhambi imeonekana kuwa ni kitu cha kawaida sana lakini ukweli ni kwamba hiyo kawaida ipo kwa wanadamu tu lakini kwa Mungu bado msimamo uko pale pale.
DHAMBI NI NINI?

Dhambi ni uasi dhidi ya sharia za Mungu =1YOHANA 3:4 mtu anapotaka kuijua dhambi hana haja ya kuuliza uliza kwa watu hana haja ya kuuliza uliza kwa Mtumishi yoyote yule kwasabu hata mtumishi anaweza kudanganya akataja dhambi zisizomgusa yeye lakini dhambi inajulikakana kwa kuzijua sharia za Mungu hivyo basi ili kuweza kujua kuwa dhambi ni nini ni lazima kupima kwa kutumia mmsheria za Mungu kwa hiyo kitendo chochote au maneno yoyote yale yanayopinzana na sharia za Mungu hayo ni Dhambi tena nasema kwa msisitizo chochote kile ambacho hakiendi sawa na maagizo ya Mungu ni dhambi haijalishi ni nani anakisema au kukifanya haijalishi ni Mtume Nabii Mchungaji Mwalimu Mwijilisti hicho sio kigezo hata kidogo kigezo vyeo hivyo sio kipimo hata kidogo bali kipimo ni neno la Mungu. Sasa basi hili ni jambo la muhimu sana kulijua kila mtu anapaswa kujua hii awe Mkristo au mpagani anapaswa kujua hili kwamba kipimo sio mtume wala nabii kipimo ni neno sasa dhambi ni kuasi maagizo ya Mungu.

Mtu yeyote yule anayefanya mambo kinyume na maagizo ya Mungu huyo mtu NI MALI YA SHETANI haijalishi ataitwa kwa cheogani cha kiroho haijalishi bado huyo mtu ni mali ya shetani na kwa kuwa yeye ni mali ya Shetani ni wazi kabisa na wote wanaomsikiliza nao ni hivyo hivyo ni mali ya Shetani kwa sababu maandiko yanena wazi wazi kuwa Atendaye dhambi ni wa ibilisi. Kutokana na sababu hiyo mtu wa ibilisi atafanya mashauri ya ibilisi. na moyoni mwake hakutatoka mambo mzuri bali siku zote atafanya mambo mabaya kwasabu moyo wake umejaa mawazo mabaya tu.
ALIYEZALIWA NA MUNGU HATENDI DHAMBI =1YOHANA 5:18.
Aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi kwa sababu uzao wa Mungu unakaa ndani yake. Hapa kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza nacho ni hiki Kuna kuzaliwa na Mungu na kuna kuzaliwa na shetani kwasabu kama Roho anasema aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi basi bila shaka kabisa wapo waliyozaliwa na shetani hivyo kama kuzaliwa na Mungu kupo basi na kuzaliwa na ibilisi nako kupo na kama. Aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi basi ni wazi kabisa kuwa anayetenda dhambi amezaliwa na shetani kwa hiyo Mtu yeyote ambaye ni Mwongo,
Tapeli,Mzinzi, Mwasherati,Muuaji, Mchonganishi, Mshirikina, Msoma nyota, Aliyeachana na mume au mkewe na kuoa au kuolewa tena, Asiyelipa madeni, Aliyedhurumu Mali za mjane na yatima, Mwabudu sanamu, Anayevaa mavazi yasiyoipasa jinsia yake, Anayejikoboa ili kuusahihisha uumbaji wa Mungu, Muuzaji mafuta na maji ya upako, Muuzaji sabuni na vitambaa vya upako, Mtume na nabii wa uongo, Mchungaji na Mwalimu wa uongo, Anayeombea watu kwa kutoza pesa, Anayenunua mafuta na kingine chochote cha upako kinachouzwa,

Na mengineyo yote yafananayo na hayo yoote wanaoyatenda hayo ni watoto wa ibilisi ni UZAO WA SHETANI, na wote wapo njiani kuelekea motoni.
TENGENEZA NA MUNGU SASA HIVI
Kama wewe uliyekutana na ujumbe huu ni unazo tabia kama hizo ujue hakika kabisa wewe ni Mwana wa ibilisi na unahitaji kutengeneza na Mungu neema ya Mungu bado ipo mlango wa neema haujafungwa bado unayo nafasi ya kutengeneza sasa basi tubu leo

Kama wewe ni Mtumishi unayetapeli watu unajijua kabisa kuwa bado hajaokoka bado kabisa tena huna wito bali umeingia kwa tamaa na umesababisha kanisa kutukanwa mimi nakwambai kuna kifo kibaya cha aibu hakipo mbali na wewe kabisa kama hautatubu leo unaenda kuaibika vibaya sana na mbaya zaidi moto wa jehanam unakungoja wale funza wa jehanam wanasubiri nyama yako utaponea wapi tubu leo tubu leo tubu leo sasa hivi mara moja na Yesu atakusamehe na kufungua ukurasa mpya wa maisha yako.
Na kwako wewe ambaye bado hajaokoka unajijua mwenyewe pamoja na kuwa na dini yako Kubwa mnasali kwenye hekalu kubwa lakini unadhambi mwenyewe unajijua sasa basi nafasi ipo leo hebu fwatisha maneno haya hapa Chini
SALA YA TOBA
Eee Bwana Yesu nimetambua kuwa mimi mimi ni mtu ninayeishi na dhambi moyoni mwangu nakuomba leo unisamehe dhambi zangu zote unisafishe kwa Damu yako niwe safi dhamiri yangu nazitubu dhambi zangu zoote kwa kumaanisha kuziacha kabisa, sitozitenda tena namkataa kabisa Shetani na kazi zake zote na laana zake zote na matatizo yake yote. Kuanzia leo nafanya agano na wewe Yesu kwa Damu yako ya agano la milele, Ahsante kwa kunisamehe amina.

BAADA YA KUOKOKA
Baada ya kuokoka sio vema kuishia hapo
Bali unapaswa sasa kutafuta mafundisho ya neno la Mungu ni lazima upate mwalimu mzuri mwaminifu atakayekulea kiroho hadi kufikia hatua ya kuweza kusimama mwenyewe kwa miguu yako na kama unapenda kuwasiliana nami kwaajili ya kukujenga zaidi kiroho
Nitafute kwenye WhatsApp kwa no hii hapa 0767 503054

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni