Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Profesa Jumanne Maghembe –
Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa
Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa
kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa
kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa
Mbunge)
5. Mheshimiwa Hamad Masauni –
Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa
kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na
Mawasiliano
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania
wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee
kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni