YESU NI JIBU

Alhamisi, 24 Desemba 2015

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA KRISMASI YAPIGWA MARUFUKU HUKO NCHINI SOMALIA KWA HOFU YA KUSHAMBULIWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA ALSHABAB

Wakati wakristo kote duniani wanaadhimisha kuzaliwa kwa Bwana Yesu Mwokozi wao huko nchini Somalia hali imekuwa tofauti baada ya serikali ya nchi hiyo  kupiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mkurugenzi mkuu katika wizara ya maswala ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

Hii inatokea baada ya kuonekana kuwa taifa hilo idadi kubwa ya wananchi wake ni wa dini ya kiislamu,hivyo kusababisha kuwepo kwa hofu ya kushambuliwa na kundi la kigaidi la Alshabab.

''Maafisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yeyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiofungamana na dini ya Kiislamu.'' alisema Sheikh Mohamed.

Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika AU iliyoko mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
 Na wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.
Chanzo BBC.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni