YESU NI JIBU

Jumatatu, 5 Mei 2014

MAMBO YA KUSHANGAZA NA AJABU KILA KUKICHA DUNIANI,NA HII NI KALI YA KTOKUAGA KWA MUDA WA MIAKA ZAIDI YA KUMI:



MTU AMBAYE ANADAI KUWA AMEPATA AGIZO LA KUTOKUOGA KWA MUNGU SASA HILI NI KWELI AMA TAYARI IMANITOFAUTI INAENDELEA KUJIKITA DUNIANI.
Bila shaka  ulishawahi kusikia au kushuhudia watu wa  jamii mbalimbali wakimlazimisha mtu mwenye matatizo ya akili  kuoga kwa nguvu kwa sababu ya kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mtu anayefahamika kama mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo, Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga tangu mwaka 2001 kwa madai kuwa alipokea amri kutoka kwa  Mungu ikimtaka afanye hivyo na ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya vinywaji.
Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga mchungaji huyo hatoi harufu na ni vigumu kutambua kuwa hajaoga hadi akuoneshe mwenyewe vielelezo!
Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati lilipomkumbusha kuwa mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia asioge:
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi. Mwaka 2000 mwanzoni Mungu aliniambia niache kuoga, na nijitenge na mke wangu na kwamba natakiwa kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo.
"Mtu yeyote ambaye Mungu anataka kumtumia kwa sababu hapa duniani, kuna gharama ambazo zimeambatanishwa  na witohuo. Kwa hiyo ninaamini kwamba hiyo ni gharama ninayolipa alisema mchungaji Olanguji. Ninavyoongea na wewe hivi sasa, sijaoga, kama unataka nikuoneshe ushahidi nitakuonesha kama una shaka juu ya haya yote nisemayo; sijaoga tangu mwaka 2001 hadi wakati huu." Kwa sasa ndugu msomaji wa blog huu ni wewe kujipanga na kuchagua kufuata imani ambayo ni sahihi la sivyo utajikuta kuwa umeingia katika mikono isiyo salama.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni